Timu ya taifa ikifundishwa na wachambuzi, nina imani tutacheza world cup

simba wa dodoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
928
Reaction score
1,012
Habari za wakati huu ndugu zangu, nina imani mpo salama pitia kichwa cha hapo juu hivi tunasubiria nini kumkabidhi MWL Kashasha kupewa timu ya taifa akafundisha, huyu jamaa ukimfatilia akiwa anachambua mpira hakuna asiko kijua hasa lugha ya kimpira
kocha wa makipa akipewa edo kumwembe nadhani makipa wa taifa stars watakua bora kama akina Buffon, Casilasi, Peter Schmechel na Dida.

Benchi la ufundi awepo Alex Lwambano na Shafii wazee historia wanaousoma mpira wa wapinzani kabla hujaanza, tukiingia ni ushindi maana jamaa wanajua historia ya mpira tofauti na historia ya Kinjikile Ngwale.

Kamati ya ushindi apewe Maulid Kitenge, Maestro, Oscar, Amri Masale na Mbwiga. Kwa hii safu nakwambia hata Taifa stars tucheze na malaika tunashinda. I tell u my friends tutaogopewa duniani.
 
Kama vile mchambuzi WA TBC MWALIM Kashasha napenda sana maekezo yake ya uchambuzi
 
Hao walijaliwa tu maneno ila hamna kitu nikama waswahili wegine ujuaji mwingi vitendo sufuri
 
Mungu kamjalia kila mtu na kipawa chake kwa hiyo ni vizuri mchambuzi abaki kuwa mchambuzi, kocha awe kocha, kiongozi awe kiongozi, shabiki awe shabiki ndio tija itapatikana. Tumeshaona wachambuzi wazuri kama akina Garry Neville au Sunday Oliseh walivyochemka walivyopewa nafasi ya ukocha.
 
... na ndio maana sikutaka Ally Mayay awe rais wa TFF kwa kigezo cha uchezaji au uchambuzi wa soka, bali angetumia zaidi sifa za uongozi wa taasisi, halafu hayo ya kuujua mpira yawe kama added advantages. Bahati mbaya wapambe wake walikuwa wmeelekeza nguvu kwenye added avantages, wakasahau kuwa si washabiki wa soka waliopo ndani ya mfumo rasmi wa wanaoingia kupiga kura, bali ni wajumbe wa mkutano wa uchaguzi
 
Shida inakuja pale ambapo vitendo ndio vinahitajika dhidi ya maneno ya uchambuzi..Pale uwanjani nyie paoneni tu
 
mwalimu kashasha ameenda shule anaongea lugha za kimpira kabisa hao wengine ni kama watangazaji wa clouds tu maneno na uchangamfu ndo vinawafanya waonekane Edo na shafii ndo zerooooooo
 
Heading tu imenitabasamisha! [emoji4] [emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…