Kukua kwa sekta ya michezo nchini Hadi kufikia viwango Bora na vya kiushindani kimataifa inawezekana na hadi timu yetu ya taifa (Taifa stars) kushiriki kombe la dunia haitakuwa ndoto Bali itakuwa uhalisia na kawaida kushiriki michuano hiyo, hayo yote ili yaweze kufanikiwa yafuatayo Ni muhimu kuongeza na kurekebisha katika sekta ya michezo.
Serikali kutenga bajeti kubwa katika sekta ya michezo; kwa maono yangu naona bajeti inayowekwa kwenye sekta ya michezo Bado haikidhi uhitaji kwenye sekta ya michezo, unakuta Bado tuna viwanja vichache vya michezo pia hatuna teknolojia za kisasa za kimichezo ili kusapoti sekta ya michezo kufikia malengo, hivyo basi kwa kuongeza bajeti kwenye sekta ya michezo tutaweza kufikia malengo yetu ya kukuza sekta ya michezo nchini.
Kuanzisha ligi za watoto wadogo; hii itasaidia kusaka vipaji vya watoto angali wakiwa wadogo, kipaji Cha mtoto huwa kinaonekana angali akiwa mtoto na baadaye huaribiwa na kupotea kabisa kutokana na mazingira mtoto anayolelewa, hivyo basi ili kutopoteza vipaji vya watanzania watoto serikali kupitia sekta ya michezo ianzishe ligi za watoto wadogo kusaka vipaji, na baadaye kuwachukua na kuwasapoti katika kuwaweka katika Academy za watoto za kimichezo.
Picha na: www.zanzinews.com
Mfano leo hii Lionel Messi Ni mchezaji Bora zaidi Duniani, lakini kipaji chake Kilionekana angali mtoto Leo Ni msaada mkubwa kwenye timu yake ya taifa ARGENTINA, hivyo basi naamini mtaani huko Kuna watoto wanna vipaji vya michezo anuwai serikali Haina budi kuwachukua watoto hao na kuwasapoti.
Picha na: Mtanzania Ltd- Dr Fledrick Mashili.
Mpira wa miguu ufundishwe mashuleni; kuanzia ngazi ya shule ya msingi Hadi Chuo somo la mpira wa miguu lifundishwe, tukianzia ngazi ya msingi mtoto atakuwa anakuwa huku anajua mpira vizuri wa darasani, atafahamu sheria zake, kanuni zake, na mbinu zake, kwa kufundishwa la mpira tutazalisha wachezaji wazawa wenye kuujua mpira wa kufundishwa darasani.
Picha na: nyakasagani: blogspot.com
Walimu waliosomea mpira wa michezo hasa mpira wa miguu waajiriwe kufundisha michezo mashuleni; shule nyingi nchini Tanzania unakuta walimu wa michezo ni walimu ambao hawana taaluma ya michezo, mfano mwalimu wa hisabati, biolojia, au uraia yeye ndo anapewa kusimamia michezo shuleni, hili linaathiri Sana kupata wanamichezo wenye ustadi wa hali ya juu, kuliko kupata walimu wenye taaluma ya michezo kwa kusomea hii itasaidia kupata wanamichezo wenye ubora na ustadi wa hali ya juu.
Kuongeza kujenga viwanja vya kisasa vyenye miundombinu ya kisasa; serikali kupitia wizara ya michezo inaweza kuongeza viwanja vya michezo kwa kila Mkoa uwe na viwanja vikubwa angalau viwili, pia kuboresha na kukarabati viwanja vilivyopo kuviwekea teknolojia ya kisasa, viwanja vya michezo vikiwa vingi wachezaji watapata maeneo ya kujifunzia michezo kwa vitendo.
Kudumisha na kuziwezesha ligi za michezo mashuleni; Kuna ligi Kama UMISETA na UMITASHUMITA hizi ligi ni za muhimu Sana kupata wachezaji Bora na wenye vipaji tishio, serikali Haina budi kusapoti ligi hizi na kuziendeleza kikamilifu, pia kamati ya utafutaji wa wachezaji wa timu ya taifa iwe inahudhuria ligi hizi kusaka vipaji na kuwachukua wachezaji Bora Kama sehemu ya kusaidia taifa letu.
Kutengeneza mahakama ya kimichezo ( TANZANIA SPORT COURT); Hii mahakama itahusika na kuhukumu masuala yote yahusuyo michezo, ikiwemo wachezaji kutokulipwa, mikataba ya wachezaji bandia, dhuluma, utapeli, pia itahusika kusuluhisha migogoro ya wanamichezo na kuhukumu viongozi wa kimichezo wanaokiuka taratibu zilizowekwa kisheria, maana miongoni mwa yanayofanya tusieendelee kimichezo Ni kukosa nidhamu kwenye michezo na ujanja kwenye sekta ya michezo.
Kuepuka njia za mkato kutafuta wachezaji wa timu ya taifa; suala la Rushwa, mjuano wa undugu, ujomba na ushangazi ni vitu vinavyorudisha nyuma sekta ya michezo nchini, vipaji vitafutwe kwenye ligi za watoto, mashuleni, ligi za ndani, kuliko kuwekana tu.
Kamati za hamasa ziwe na wanamichezo kindakindaki na sio mashabiki. Mrisho Ngassa atakuwa na nafasi nzuri sana ya kumshauri Mzize pamoja na kumpa hamasa kuliko Baba Levo ambae atamsifia tu muda wote. Kamati za hamasa za timu za Taifa ziwe na wachezaji wakongwe pamoja na makocha wazawa. Hawa wote wanaweza kuwa na mbinu za kivita za kuivusha Stars kuelekea katika dunia ya ahadi.
Wachezaji wawe wanapewa motisha; Motisha ni muhimu sana kwa popote pale. Makazini kuna motisha, Mashuleni kuna motisha nakadhalika. Hivyo hata kwa wachezaji wanahitajika kupewa motisha kwa lengo la kujituma zaidi. Mfano Rais Magufuli aliwahi kuwapa wachezaji wa Stars viwanja Dodoma baada ya kufuzu AFCON baada ya kupita miaka mingi bila kufuzu. Ni kuweka mikakati sahihi na kuzingatia mbinu nzuri za kutoa Motisha kwa wachezaji.
Sekta ya michezo ishirikiane vyema na TFF; Ushirikiano mzuri baina ya shirikisho "TFF" Pamoja na wizara ya Michezo. Hizi ni pande mbili ambazo zinatakiwa kuwa bega kwa bega. Jambo la Wizara katika muelekeo wa michezo shirikisho linatakiwa wafahamu na jambo la shirikisho wizara ya michezo pia wanatakiwa wafahamu muda wote. Hawa ndio wao wachora ramani wa mjda wote wa namna gani Mipango ya Stars itaenda.
Kuwapa Uhuru wa kutosha wadau wa michezo; Upande wa wadau. Hawa ni watu muhimu sana kwenye sekta ya michezo kwa matokeo mazuri ya timu ya taifa. wadau hawa ni kama waandishi wa habari za michezo, Wachambuzi, Makocha na wachezaji wa zamani.
Hawa watashauri pale inapohusika, Watakosoa pamoja na kusifia pia pale itakapohusika. Na hawa ndio watakuwa washika dau muhimu kwaajili ya kupeleka ajenda ya stars kufanya vema.

Upvote
2