Timu ya Taifa ya Riadha kutuwakilisha All African Games, Ghana
Timu ya Taifa ya Riadha wameondoka leo na kuagwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania Silas Lucas Isangi na Kaimu katibu mkuu wa RT Wakili Jackson Ndaweka katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
Wanariadha hao 8 wakiwemo wa Mbio za Uwanjani, Mbio ndefu na Mrusha mkuki, wameondoka kwenda Accra , Ghana kushiriki mashindano ya Afrika “All African Games” ambayo yanafanyika huko na yalianza toka tarehe 8 na yataendelea hadi tarehe 23 Machi 2024.