Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni yawasili Misri

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
252
Timu ya Taifa ya soka la Ufukweni (Beach Soccer) imewasili salama jijini Cairo nchini Misri tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli.

Msafara wa timu ya soka la Ufukweni ulipokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania waliopo nchini Misri, pamoja na viongozi wa chama cha soka nchini Misri (EFA).

Leo jioni kikosi kinatarajia kufanya mazoezi mepesi, kabla ya kesho kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja utakaofanyika mchezo siku ya jumapili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaitakia kila la kheri timu ya soka la ufukweni katika mchezo wake wa marudiano siku ya jumapili dhidi ya Misri.

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…