Timu ya wanawake ya Simba yashinda kombe ligi kuu msimu wa 23/24 chini ya kocha Mgunda

Timu ya wanawake ya Simba yashinda kombe ligi kuu msimu wa 23/24 chini ya kocha Mgunda

Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
2,824
Reaction score
2,264
Baada ya vuta nikuvute ya hapa na pale kati ya wababe Simba, Yanga na JKT, hatimaye timu ya Simba wanawake wameibuka mshindi wa kombe hilo la Ligi kuu wanawake baada ya kuifunga Alliance girls ya Mwanza kwa bao tatu kwa nunge.

Ushindi wa timu hiyo umechagizwa na uhodari wa kocha Juma Mgunda ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho kabla ya kubeba mikoba ya kocha Benchika.

Hongereni sana Simba Queen walau mmeonyesha njia.

IMG_20240608_104453.jpg
 
Usiseme Juma Mgunda, Sema Pep Guardiola mnene

Mzee wa boli linatembea 👏👏🙌
 
Hili likikosa parade basi Mangungu na Try waondoke mazima
Sisi mashabiki tunataka parade lianzie popote ila lipite pale jangwani na liinuliwe na Fetty dancer na korazone
 
Hatimaye timu ya Simba yashinda kombe ligu kuu msimu wa 23/24 chini ya kocha Mgunda

Sio HATIMAYE, hiyo ligi ya Women inajulikana kuwa bingwa wa mara zote anapaswa kuwa ni Simba, na miaka ambayo Simba sio bingwa ndio unaweza kuandika HATIMAYE SIMBA AKOSA UBINGWA
 
Sio HATIMAYE, hiyo ligi ya Women inajulikana kuwa bingwa wa mara zote anapaswa kuwa ni Simba, na miaka ambayo Simba sio bingwa ndio unaweza kuandika HATIMAYE SIMBA AKOSA UBINGWA
Simba si hata bingwa mtetezi wa kombe hilo. So hatimaye bado inaswihi.
 
Back
Top Bottom