Timu Zach VPL zianzishe timu za wanawake

Turnkey

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
7,359
Reaction score
5,837
Kwanza naipongeza timu ya Tanzania Queens kwa kutwaa taji la challenge mjini Jinja Uganda. Ila ombi langu ni kwa vilabu vya VPL kuanzisha timu za soka la wanawake. Timu kama Yanga. Simba na Azam na nyingine zenye uwezo zinaweza kufanikisha ili zoezi. Ukitazama vilabu vya ligi kuu uingereza Wana timu za wanawake hivyo uleta hamasa. Kitendo cha TFF kuhamasisha timu za mitaani ndio zianzishe timu za kuingia kwenye ligi ya taifa ya wanawake ni makosa makubwa. Mpira wa wanawake kuna soko kubwa la wachezaji katika nchi za Scandinavia. Germany na USA. Hivyo basi timu zetu zinaweza kukuza vipaji na kwenda kuwauza wachezaji katika nchi hizo. Wewe Mimi ni yule tujiunge kwa pamoja kuinua huu mchezo wa wanawake. Alamsiki
 
Zimeambiwa tayari na wanadai Kutakuwa na ligi ya wanawake sasa sijui litatekelezwa au vipi mana maneno ni mengi kuliko vitendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…