Timu zetu ziache ubabaishaji. Kocha mpya, benchi jipya, wachezaji wapya?

Timu zetu ziache ubabaishaji. Kocha mpya, benchi jipya, wachezaji wapya?

EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
1,230
Reaction score
1,352
Miongoni mwa sababu soka letu halikui ni huu utaratibu wa klabu zetu (hasa hizi 3/kubwa) kutimua makocha bila kuwa na mipango sahihi baada ya hapo.

Kuhusu wasaidizi wa kocha.

Kimsingi kocha anapaswa kuteua wasaidizi wake. Hii hupelekea mambo mengi; heshima, kuaminiana, kujituma, nk na hivyo benchi kuwa na chemistry nzuri.

Kinyume chake ni benchi kutokuwa na chemistry nzuri. Mfano ni timu ya Azam. Kila uchao kocha mpya benchi lilelile. Majungu hayaishi. Pesa ipo lakini sijui ni mafanikio gani Azam inaweza pata.

Ulaya kuna timu kama United. Waliona aibu kumtimua Jowzey na benchi zima. Wakawabakiza Carrick na McKiena ambao hawakubaliani na displine/commitment ya baadhi ya wachezaji (Pogba/Martial). Matokeo yake unaweza (kama unajua mpira) timu hucheza kana kwamba OGS ana mshauri mmoja tu (Mike Phelan). Timu ina mbinu moja tu; kuwazidi mbio wapinzani.

Kuhusu kikosi (wachezaji wapya).

Kwa kawaida tabia na hulka za binadamu ziko very complex. Pia kocha mpya ni dhahili ataingia na mbinu/mifumo mipya ambayo itawasukumia mbali baadhi ya wachezaji (atataka kikosi chake).

Hivyo timu zinapotimua makocha zijue kabisa kuna wachezaji kocha mpya atataka aletewe na kuna wengine atataka waondoke. Angalia project zilizofanikiwa (City, Liverpool).

Kinyume chake ni kuwa kulazimisha kocha mpya afanye kazi na wachezaji waliopo au wachezaji kusajiliwa na uongozi (akina Haji Manara) badala ya kocha mwenye migongano haitaisha kikosini. Unaweza ona Mourinho aliyekuwa akimlilia Danny Rose akiwa United, ameshindwa kufanya naye kazi Spurs!

Timu kama Arsenal au United (hasa Arsenal) ni ngumu sana kufanikiwa uwanjani kwani kocha lazima afanye kazi na kikosi kilichopo. Wakiongezwa wachezaji ni wawili watatu wa hapa na pale.

Kwa Simba nilidhani MO anadhamira ya dhati ya kupata mafanikio ya uwanjani ila kwa sasa nina walakini huenda lengo ni biashara tu (rejea wafanyabiashara walivyoziharibu United, Arsenal na AC Milan).

Au labda MO ni tajiri/mjasiriamali asiyejiamini (kuhusu uendeshaji wa klabu) hivyo ameamua kuwakabidhi wababaishaji akina Kaduguda, Manara, nk watumie hisia zao kuendesha klabu.

Hitimisho

Timu inapofanya uamuzi wa kutimua kocha ijue inaingia kwenye project nyingine kabisa. Hivyo uamuzi wa kutimua ni bora usifanyike ikiwa hakuna plan sahihi (rejea suala la Ausems). Timu zisihadaike na viapo vya makocha kuwa watafanya kazi na kikosi kilichopo kwani kiuhalisia hilo haliwezekani. Mfano ni OGS ambaye kwake ile ilikuwa dream job hivyo chochote kwake ilikuwa YES.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachoongea ni kweli ila kwa Tanzania wawekezaji wetu wapo kifedha zaid wanahitaji mafanikio ya haraka na kusikiliza mashabiki zaidi wanachokitaka ambao kila kukicha wanakuja na jambo jipya .Mashabiki wanapenda leo wafanyiwe kitu flani wakifanyiwa wanaugeuka tena uongozi mfano Uchebe baadhi ya mashabiki hawakumtaka mpaka kumrushia makopo Kule Mwanza leo hii wanamlilia arudi eti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azam kuna mtu anaitwa Iddi Cheche, kocha yeyote anayeajiriwa Azam lazima afanye naye kazi (atake au asitake)! Sijajua sababu! Bado matajiri wa bongo hawajawekeza vilivyo katika soka, hata hawa kina Mo na Bahresa ni kama wanazuga zuga tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom