Juma jaibu kuhanga
New Member
- May 18, 2024
- 4
- 5
Suala la rushwa na kudhibiti kwake bado kuna ugumu na changamoto kubwa licha ya jitihada zinazofanywa na taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa hapa nchini. Suala la rushwa ni moja ya kikwazo ambacho kinakawamisha maendeleo katika jamii yeyote hile kwani inazuia haki ya watu wengine. kuna mambo kadhaa yakiafanyika natuamaini hili suala la rushwa litapotea au kupungua kwa kasi zaidi, kama yafuatayo;
Viongozi au Taasisi ziweze kuwaripoti wale watu ambao wanawashawishi wao kupokea rushwa, Ni vigumu au nadra sana kumuaona kiongozi anasimama na kusema kuna mtu kanishawishi nipokee rushwa kwa ajili ya jambo fulani lakini viongozi ndio pekee wanapewa lawama za kuomba rushwa. Hivyo suala la kiongozi kuripoti watu wanaotoa au kuwashawishi wao kupokea rushwa litapunguza mazoea ya baadhi ya wadau kutoa rushwa kwa kuhofia mikono ya sheria.
Pia hukumu ya kupokea na kutoa rushwa ifanyiwe marekebisho(reform). Inaweza ikawa vitendo vya rushwa vinaongezeka kila siku wa sababu ya udhaifu wa sheria. Hivyo basi mamlaka husika ziweze kutunga sheria maalum ya makosa ya rushwa bila kujali kiwango cha rushwa alichopokea au kutoa mtu yaani kuwepo na hukumu moja kwa wanaotoa rushwa mfano mtu akipokea au kutoa rushwa atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela bila kujali kiwango cha rushwa yake. Hii itasaidia kupunguza rushwa katika taasisi mbalimbali.
TAKUKURU iweke wazi changamoto wanazopitia katika kazi zao kwa wananchi ili kupata ushauri na njia mbadala za kutatua. Jamii ni wahanga wa matukio yote hivyo jamii ndiyo inayojua njia mpya ya kutoa na kupokea rushwa kila kukicha yaani takukuru wakitumia njia hii wao Wanatumia njia nyingine hivyo kufanya hivyo itasaidia kuondoa baadhi ya vikwazo kwa kushirikisha jamii.
Serikali na TAKUKURU ziandae midahalo na mijadala mara kwa mara ambayo itawashirikisha wananchi moja kwa moja.Ukusanyaji wa maoni na hoja kupitia midahalo itasaidia upatikanaji wa masuluhisho katika uboreshaji wa mapambano dhidi ya rushwa.
Pia serikali iboreshe huduma za kijamii kwani watu wengi wanatoa rushwa kwa sababu ya uwepo wa wahudumu wa chache katika sekta mbalimba watu wanatoa rushwa ili kuepukana na foleni ambazo zinakua kikwazo na kero kwa baadhi ya wananchi kwani wanaona ni bora kutoa rushwa ili kuepikana na adha ya kukaa foleni.
Pia serikali itoe posho kwa wahudumu wa huduma za kijamii, wahudumu wengi upokea rushwa kwa sababu ya kutokidhi kwa mishahara yao hivyo basi wanaona kama rushwa ndio njia pekee ya kujipatia posho ili kuweza kumudu gharama za maisha yao.
Pia vianzishwe vyuo vinayotoa kozi za kupambana na rushwa kuanzia astashahada,stashahada na shahada.Hii itasaidia kiwakuza vijana na kuwa wabobevu katika utendaji wao wa kazi dhidi ya hii rushwa. kwani nchini hakuna chuo cha rushwa ambavyo vinatoa kozi hii muhimu katiaka ngazi ya stashahada na kuendelea.
Kuamasisha matumizi ya utoaji na upokeji wa fedha kwa nji ya risti hili kuepuka mianya ya rushwa nchini,suala matumizi ya risti badala ya cash money katika taasisi za umma ni vyema zaidi katika kuongeza ufanisi na kuzuia tamaa ya viongozi na wananchi kwa ujumla.
Mwisho; serikali iunde spy network katika kila sekta ili kufuatilia uondeshaji wa sekta hizo bila kutoa rushwa na kuwafichua wanaopokea rushwa katika taasisi husika.

Upvote
5