stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,216
- 26,225
Mnaojua tufahamishane,masikio yangu yanapiga kelele,yaani ni kama miluzi ila inapiga mingi na sauti tofauti-tofauti kama vile kelele za mgonjwa alietumia dawa ya Quinine,nimepimwa masikio hayana tatizo lolote nilichoambiwa ni kuwa kutokana na kazi niliyokuwa nafanya ni ya mkelele ina wezekana imenisababishia hiyo hali na kiasi fulani imenipunguzia hata uwezo wangu wa kusikia,tabibu wangu akaniambia ugonjwa huu unaitwa tinitus na siwezi kupona,sasa kuna yeyote mwenye kufahamu dawa ya maradhi haya anisaidie.