Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Najua wengi tunapika na wengi tunajua kupika. Leo nimeona ni vema nikupe tip juu ya Tangawizi na Vitunguu Swaumu, kwani mbali na viungo hivi kuwa na virutubisho muhimu sana katika miili yetu pia ni viungo vizuri sana katika mapishi yetu ya kila siku.
Kama unataka kuleta mabadiliko katika chakula chako anza kutumia hivi viungo kwa kufanya kuwa ni muhimu katika mapishi ya mboga zako zote.
MAHITAJI
JINSI YA KUANDAA
Andaa mahitaji hayo kwa kuondoa maganda ya vitunguu swaumu, menya maganda ya tangawizi, kisha kata kata ziwe ndogo ndogo weka katika kinu chako au ile mashine ya kusagia kwa walionazo. Ongeza chumvi kidogo na pili pili kwa wale walaji wa pilipili. Twanga kwa pamoja vilainike kabisa / saga hadi vilainike.
Baada ya hapo waweza hifadhi katika friji lako, na ukawa unatumia kila mara unapounga mboga zako. Na hii huwa hivi weka mafuta yako weka vitunguu kisha chota kijiko kimoja cha chakula weka kwenye hivyo vitunguu kaanga kwa pamoja hadi viive kisha endelea na kuunga mboga yako. Amini nakwambia ladha ya mboga zako itaboreka na kuwa tamu sana.
Vile vile Tangawizi peke yake yatumika katika kutengeneza juisi hivyo wachukua vipande kadhaa vya tangawizi na unachanganya katika kuisaga juisi yako na utapata ladha nzuri na harufu nzuri sana.
Kitunguu swaumu pia unaweza kukitumia katika kupika wali &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Menya punje kadhaa ziponde kidogo tu kisha chemsha katika maji yako ya wali , mara maji yakisha kuchemka ondoa vitunguu swaumu katika maji kisha weka mchele wako upike kuwa wali. Naam wali utakua na harufu nzuri sana na unakua unavutia kula.

- Vitunguu Swaumu
- Tangawizi
- Chumvi
- Pilipili ( Kwa wanautumia pili pili)