Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 142
Wakuu,
Nimesikia habari za kutatanisha ama kusikikitisha kutoka kwa mtu wangu wa karibu,kwamba huyu Jamaa Athuman Tippo (Another True Cebebrity wa Kibongo),anakashfa nzito ya mpaka imefikia kutangazwa kwenye Radio ya Clouds Fm. wiki iliyo pita.
Kisa ambacho sikukielewa vizuri,sasa kama kuna mtu anajua kwa undani nini kimelitokea mpaka ikawa hivyo ilivyo kuwa tafadhali embu tuwekee hapa,alafu by the ways,yule dogo aliye peleka hiyo habari ambaye ndio mwenye hilo beef na Tippo nasikia ana Blog,sasa kama hivyo ndivyo mwambieni au alete kisa chao hapa tujue maana wengine sio watu wa Radio.
Kwani wewe umehadithiwa nini na huyo mtu wako wa karibu? Maana hoja yako bado haijaeleweka vizuri. Eleza kashfa yenyewe kwanza nasi tupate pa kuanzia!
Siwezi kusema kitu ambacho sikijui,ndio maana nikaomba watu walio sikia Radioni ama wenye kujua waniambie.
Kwanini nilete majungu hapa wakati kuna walio sikia?
Ina maana rafiki yako hakusikia kitu redioni, na je alikupa habari gani? Mwanzoni umedai umehadithiwa, sasa unakana! Kulikoni Sanda Matuta?
Nadhani hajafanya vibaya, na huo upembuzi ndo anaufanyia humu. Mbaya ni kumwaga kila kitu wakati huna uhakika. Tusubiri waliosikia, kama hawapo thread ifungwe.Mkuu Sanda Matuta,
Unaonaje kama ungefanya upembuzi wako kwanza halafu ndiyo ukaja na thread yako hapa?
Nadhani hajafanya vibaya, na huo upembuzi ndo anaufanyia humu. Mbaya ni kumwaga kila kitu wakati huna uhakika. Tusubiri waliosikia, kama hawapo thread ifungwe.
we santa acha kuleta issue za kitoto,huyo rafiki yako kam hukumuani mimi utaniamini vipi??mi nilisikia Tippo kamla blue ndio hiyo??[/QUOTE]
Mkulu,
wewe ndio haswaa... umepituka!
Ok lakini hayo ni mambo yako umesikia wewe (sisi wabongo Hodari sana kusema watu hasa wakiwa na mafanikio kidogo)si ajabu baadae kidogo kasema pia Kamla Mangwea au Hata Bushoke kwani hao pia wako kwenye label yake.
Nilicho taka kujua mimi ni kuhusu huyo kijina Choka amabye anasema kanymwa nauri na yeye ni mwajiriwa wa Zizzoue Fashiona mpaka kaenda radio kwa hiyo issue......
ahahahaha...nilisikia hiyo habari ya zizzou entartaiment na dogo m1 anajiita dj choka ...issue naona ni utoto, ujinga na kutokujua nini maana ya mkataba/terms za mkataba...
dogo anaclaim kuwa alitelekezwa na zizzou mitaa ya shule ya uhuru akiuza bidhaa za mwajiri wake siku ya mechi kati ya tanzania na kina drogba.....kwa hiyo ameamua kuacha kazi na ku-terminate mkataba wa miaka miwili uliokuwa wamakubaliana ila hawajasign...na dogo alishatumika na zizzou entartainment kwa kitu kama 3-6months....
maswali ya msingi ambayo dogo anatakiwa atujibu watu wenye akili zetu ni haya..
1-...akiwa kama dj choka...aliajiriwa zizzou akauze jezi au akapige disko siku ambazo wasanii wa zizzou wanafanya maonyesho?
2-...kama ndio (1)...kwanini alikwenda kuuza jezi..kazi ambayo ipo nje ya mkataba wake?
3-...kwanini kwa umri wake na umaarufu wake anakosa hata tsh 5000/= mfukoni ya kurudia nyumbani kwa tax (sio daldala kwa kuwa yeye ni maarufu mjini..ndio maana analalamika kudhalilishwa)
4...kutotiwa sign kwa mkataba kati yako na zizzou kisheria sio kigezo cha wewe kusema sio mwajiriwa wa zizzou...(consent Ilikuwapo ndio maana ulikuwa unalipwa mshahara...hata kama ulikuwa mdogo)...pia sio lazma mwajiri akuletee mwajiriwa mkataba utie sign...unaweza kuandaa mkataba kama mwajiriwa na kumpelekea mwajiri wako atie sign....(nadhani kijana hana lawyer au hajui umuhimu wa watu hao)
5...dogo anatakiwa pia ajue madhara ya kwenda public ku-accuse mtu..anaweza kupelekwa kwa pilato kwa defamation ya zizzou ambaye ni mfanyabiashara na kutakiwa kumlipa...(sijui kama dogo anaweza kulipa...maana hata tsh 5000 ya tax alikuwa hana)
6..dogo kama sio ujinga...unauza nguo unapata tshs say 100,000/= kweli unashindwa kutumia hiyo pesa ikurudishe ofisini na ukaelezea yaliyojiri mpaka ukarudi...ona sasa ume-jiexpose radioni kuwa hukuwa na hata tshs 1 ya kwako ila unazo za zizzou na hujui kabsaaaa kusolve matatizo yanayotokea mbele yako???
dogo atupatie majibu na sio kuropoka hovyo radion na kulialia kama kweli kaonewa na kudhulumiwa.....NI MAONI TUU WADAU
du wabongo tuna mambo sie
Hili suala la huyu kijana ni la ki maslahi zaidi, inaonekana Zizzou anawatumia hawa jamaa kwa ujira mdogo sana, ila kilichomfanya Dj Choka ashindwe kuwa mvumilivu mpaka kwenda redioni ni lile suala la kutolewa kwenye nyumba aliyokua amepangishiwa na Zizzou pale Sinza Lion, na ni mzazi wake Dj Choka aliyeokoa jahazi na kumlipia kodi ya miaka miwili.
www.djchoka.blogspot.com