Tishio la Gen Z lawanyima amani viongozi wa Afrika, wanatisha safari zao nje ya nchi. Wahofia kimbunga cha Arab Spring 2011

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Gen Z movement zilianzia Kenya, zinaelekea Uganda na sasa zimebisha hodi Nigeria. Yapo mafanikio kadhaa yameanza kuonekana kama:

1. Marais kusitisha safari zao nje ya bara la Afrika kwenda kuomba
2. Baadhi ya bajeti zimefyekwa tumeona Kenya, Uganda na hata Tanzania
3. Mabadiliko ya mabaraza ya mawaziri na vyombo vya dola
4. Watawala wameanza kupunguza dharau kwa wananchi
5. Sera za ajira zimeanza kuangaliwa upya ikiwemo sekta ya umma kutoa matangazo mengi ya ajira tumeanza afya na elimu Tz

Hali hii ya maandamano inaathiri sana utendaji wa mazoea wa serikali kama za kwetu ambazo mtu akiwa kiongozi anatamani aombewe kila saa badala ya kufanya kazi.

Je, haya maandamano yanaweza kubeba taswira ya kile kilichotokea nchi za kiarabu? Let us wait and see.
 
Watawala waache mazoea katila kuwaongoza watu. Badala ya kuwekeza nguvu kwenye miundombinu na uendeshaji wa serikali kwa anasa, wajikite kuhakikisha walau asilimia 50% au zaidi ya vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali wanapata ajira. Bahati nzuri nafasi za kazi zipo nyingi sana serikalini isipokuwa tu urasimu wa baadhi ya watendaji wa serikali ndio kikwazo kwa ajira za vijana hawa.
 
Kutegemea kazi serikalini haitatusaidia, labda tuseme waweke sera nzuri kusaidia graduate waanze baishara zao bila kulipa Kodi angalau kwa mwaka mmoja.
 
Hakika hata Mama asipoangalia maandamano hayo yataingia TZ

Yalianzia Kenya, hivi sasa yamevuka mpaka yameingia Uganda, hivi hawa watawala wetu, wanangoja Nini kurekebisha mambo?

Au wanasuniri maandamano hayo yatinge TZ, ndiyo waanze kusituka??😎
 
Hakika hata Mama asipoangalia maandamano hayo yataingia TZ

Yalianzia Kenya, hivi sasa yamevuka mpaka yameibgia Uganda, hivi hawa watawala wetu, wanangoja Nini kurekebisha mambo??

Au wanasuniri maandamano hayo yatinge TZ??😎
Vizazi vinabadilika, shida ya tawala za afrika wanadhani wanatawala vizazi vile vile vya enzi za uhuru, kumbe kila kizazi cha sasa kina demand tofauti
 
Mama ni lazima atafakari Kwa makini sana.

Huu mtindo wa baadhi ya watendaji wake kuendekea kumsifu tu kuwa mama unaupiga mwingi na yeye mama akichekekea😀

Kumbe ndiyo hao hao "wanaokomba'" mabilioni ya pesa za sisi walipa Kodi wa nchi hii, wakituachs sisi raia katika umasikini wa kutisha!

Hii nchi inebaki kuwa ya machawa wa kupitiliza, badala ya kufanya kazi Kwa weledi
 
Mama ni lazima atafakari Kwa makini sana.

Huu mfumo wa baadhi ya watendaji wake kusifu tu kuwa mama unaupiga mwingi na yeye mama akichekekea........

Kumbe ndiyo hao hao "wanaokomba'" mabilioni ya pesa za sisi walipa Kodi wa nchi hii, wanakuwa machawa badala ya kufanya kazi Kwa weledi!
Tatizo watawala wengi wa Afrika wanapenda kusifiwa!! Nachelea kusema kama kweli mama ana nia ya kutafakari! Angalia kiwango cha ubadhirifu wa mali za umma (CAG report) na hakuna hatua zinazochukuliwa! Wahusika bado wako kwenye vyeo na wanaendelea kula kama mchwa tu!
 
Huyo mama Wacha awachukulie waTZ, kuwa ni walewale wa siku zote Hadi pale mambo yamkute kama Ruto, ambaye hivi sasa anakiona kiti Cha Urais Cha moto kwelikweli😀
 
Wao wanajuwa watz wote wana akili mawazo za kina stev nyerere mondi mwijak baba level usanii usanii tu

Ova
 
Mkuu Akfrika imelaanika, hili bara ni kiza tu hata yakifanyika hayo maandamano hakuna kitakachobadilika
 
Gen Z movement zilianzia Kenya, zinaelekea Uganda na sasa zimebisha hodi Nigeria. Yapo mafanikio kadhaa yameanza kuonekana kama:

1. Marais kusitisha safari zao nje ya bara la Afrika kwenda kuomba
2. Baadhi ya bajeti zimefyekwa tumeona Kenya, Uganda na hata Tanzania
3. Mabadiliko ya mabaraza ya mawaziri na vyombo vya dola
4. Watawala wameanza kupunguza dharau kwa wananchi
5. Sera za ajira zimeanza kuangaliwa upya ikiwemo sekta ya umma kutoa matangazo mengi ya ajira tumeanza afya na elimu Tz

Hali hii ya maandamano inaathiri sana utendaji wa mazoea wa serikali kama za kwetu ambazo mtu akiwa kiongozi anatamani aombewe kila saa badala ya kufanya kazi.

Je, haya maandamano yanaweza kubeba taswira ya kile kilichotokea nchi za kiarabu? Let us wait and see.
Kama hakuna mifano ya Marais waliopunguza ziara nje ya nchi, waliopunguza dharau na kadhalika hii hoja ni muflisi!
 
Back
Top Bottom