Hali inatisha Kanda ya Ziwa
Mwaka mmoja wa uvuvi haramu watikisa uchumi, watishia kuliua Ziwa Victoria
Makokoro, nyavu hatari kutoka Uganda, Burundi vyaingizwa kwa fujo
*TAFIRI wakiri, watega nyavu kwa saa mbili ziwani na kuambulia samaki mmoja
Na Alex Kazenga
Amini usiamini, samaki wanakwisha ndani ya Ziwa Victoria, hali inayotishia afya, uchumi na hata amani kwa mamilioni ya wananchi wanaolizunguka ziwa hilo; JAMHURI linaripoti
Tishio hilo linatokana na uvuvi haramu ulioshamiri kwa takriban mwaka mmoja sasa, ukifanyika mchana na usiku bila hofu ya kuwapo kwa serikali
Akizungumza na JAMHURI, mkazi mmoja wa Kanda ya Ziwa anasema: “Hali hii (uvuvi haramu bila hofu) imeanza tangu mwaka jana.
Si hapa tu, ipo na inaonekana wazi katika wilaya za Muleba, Sengerema na Ukerewe.”
Ni aina hii ya uvuvi ndio unaozuiwa kisheria.
Ndio umesababisha kuadimika kwa samaki wa kila aina ndani ya Ziwa Victoria
Uvuvi ndio shughuli kubwa ya kiuchumi kwa Kanda ya Ziwa na kudorora kwake kunazua hofu kwa wengi.
JAMHURI linafahamu kwamba kwa takriban miezi mitatu sasa samaki maarufu aina ya sato na sangara wameadimika ziwani na kusababisha ugumu wa maisha kwa watu waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta ya uvuvi
Chanzo Gazeti la Jamhuri Aprili 19, 2022