TLP: Kudai katiba Mpya ni kuichonganisha Serikali, Katiba Mpya haipo kwenye ilani ya CCM

TLP: Kudai katiba Mpya ni kuichonganisha Serikali, Katiba Mpya haipo kwenye ilani ya CCM

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
HAIWEZEKANI Chama cha Siasa kuibuka na kusema kinataka masuala ambayo yapo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) bali wanachama waeleze changamoto katika jamii zinatatuliwa kwa njia gani?

Umoja wa Vijana Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kupitia Mwenyekiti wa Vijana Taifa TLP, Eng.Aivan Maganza ameyasema wakati akizungumza na wandishi wa habari mkoani Dar Es Salaam leo. Amevitaka vyama vya upinzani nchini kuacha kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kitendo chao cha kudai katiba mpya ili hali suala hilo halipo katika ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema kuwa kinachotakiwa ni kutatua changamoto katika jamii na si kuzungumzia vitu ambavyo havisaidii kutatua changamoto katika jamii.

"Tunachotaka ni Kwenye shida ya maji tunatoka vipi?, Kwenye mikopo ya Vijana tunatatuaje?, kuja kwenye jamii kueleza kuwa Umeme tutapelekaje vijijini, tunachotaka watoke waseme ni namna gani Reli ya Mwendo wa Haraka (SGR) inakamilikaje, watuambia mradi wa Rufiji unamalizikaje, hivi ndio vitu tunavyovitaka." Amesema Eng. Maganza

Hata hivyo alihoji Chama cha Siasa cha upinzani kinachodai Katiba Mpya, hilo fungu la fedha za kuanza kujadili Katiba Mpya linatoka wapi? Ingawa tumesikia bungeni wakati wa bunge la bajeti ya 2021/ 2021 hakuna bajeti ya kutengeneza Katiba mpya.

“Rais Samia alishasema kuwa atakutana na wapinzani, hizi haraka za wenzetu wa Chadema zinatoka wapi? huu ni wakati wa kumuacha Rais aliletee maendeleo Taifa letu ndipo hayo mambo mengine yafuate siku zote wanasiasa ndiyo wachochezi wa katiba mpya." Amesema Eng. Maganza

Amesema kuwa katika bajeti ya 2021/ 21 hakuna bajeti ya Katiba mpya hivyo kama chama cha siasa cha upinzani wasihangaika kuwasemea watanzania kuwa wanahitaji katiba mpya maana haina fungu la fedha.
Hata hivyo Eng. Maganza amesema kuwa kwa sasa vyama vya siasa viachane na dhana ya katiba mpya na waache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afanye kazi yake au wasubiri uchaguzi mwingine ndio waingine dhana ya katiba mpya.

Ameongeza kuwa wao kama TLP hawapo tayari kuona juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuijenga nchi hii zikififishwa na wanasiasa wenzao aliodai kuwa wengi wao wanakuwa na ajenda tofauti na siyo zenye lengo la kujenga na kuleta umoja wa watu wote.

Licha ya hayo Eng. Maganza ameomba Vijana wakumbukwe kupitia mikoa yao hadi ngazi ya Halmashauri waweze kuwezeshwa kutokana na fursa zilizopo huko ili wachangie Taifa kupata Pato na wao pia, hivyo amewataka wakuu wa wilaya, Wakurugenzi kusimamia hilo ili taifa lipige hatua.
 
Katiba mpya haimo kwenye ilani ya CCM. Lakini pia ikumbukwe hata magonjwa kama corona, hayamo kwenye ilani. Ninachoelewa ni kwamba hakuna mpango kazi usiokuwa na nafasi ya masuala mutambuka.

Bila shaka katika mapito ya taifa, uzoefu wetu na mabadiliko ya kijamii na kitecknolojia yanayoendelea kwa kasi duniani, serikali inaweza kuona umuhimu wa kutengeneza katiba mpya kama inavyoshughulikia masuala mengine muhimu yanayoonekana yana mashiko kwa taifa. Kama serikali ikidhamiria, inaweza kusimamia utengenezwaji wa katiba ya nchi isiyokuwa na mfungamano wa upande wowote.

Angalizo: Bunge la Jamhuri ya Tanzania, lisigeuzwe kuwa bunge la katiba. Kurudia hila za awamu ile, ni hujuma kwa taifa.
 
TLP mgombea wao wa u Rais 2025 na mama Samia?

We acha tuu. Mwendazake alivuruga akili ya wengi. Yaani najiuliza huyu poti wangu angetutawala kwa miaka mingine mitano au kumi. Sijui kama taifa lingebaki na mtu mwenye uwezo wa kufikiria. Maana almost wote tukiongozwa na Kabudi na Gwajima tulikuwa tumeshakuwa wajinga kabisa.
 
We acha tuu. Mwendazake alivuruga akili ya wengi. Yaani najiuliza huyu poti wangu angetutawala kwa miaka mingine mitano au kumi. Sijui kama taifa lingebaki na mtu mwenye uwezo wa kufikiria. Maana almost wote tukiongozwa na Kabudi na Gwajima tulikuwa tumeshakuwa wajinga kabisa.
TLP ilikua pale kuuaminisha Ulimwengu kuwa Tanzania vyama vya siasa vinapata haki sawa sawa na CCM. Baba mkwe alifika bei akanunuliwa.
 
Mercenary tu hao!! Aliwahi kuwazungumzia Mwlm Nyerere wanasiasa wa namna hii.Mercenary tu!!
 
Hivi TLP kuna mwenye akili pale kweli?
Hovyo kabisa
Kwani Katiba Mpya haiwezi kukanyangwa! Hapa cha msingi wakati wote ni utashi wa kisiasa wa viongozi wetu kuisimamia katiba. Mfano juzi JPM alipofariki katiba ya 1977 imetuvusha kupata Rais,nashauri kuipitia Katiba isiwe fashion au kufanya kwa mihemko kwa ajenda ya siri hili ni jambo kubwa
 
Back
Top Bottom