Uchaguzi 2020 TLP yasema inaendelea kumuunga mkono Magufuli. Kauli ya msajili kwamba wamesitisha uamuzi huo hawaitambui

Uchaguzi 2020 TLP yasema inaendelea kumuunga mkono Magufuli. Kauli ya msajili kwamba wamesitisha uamuzi huo hawaitambui

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
CHAMA cha Tanzania Labor Party (TLP), kimeibuka na kusema kuwa bado kina nia ya kumuunga mkono mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao.

Kimesema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania ilikosea kutangaza kwamba wamesitisha uamuzi huo.

Akizungumza na Nipashe, Makamu Mwenyekiti wa TLP, Domina Rwechngura, alisema msimamo wao upo pale pale wa kuendelea kumuunga mkono mgombea huyo.

“Sisi tuliishasema tangu mwezi wa tano kwamba tutamuunga mkono Rais Magufuli katika uchaguzi huu, hivyo msajili kauli yake kwamba tumesitisha uamuzi wetu hatuitambui,” alisema.

Hivi karibuni vyama vya TLP na UDP viliripotiwa kujiondoa mpango wa kumuunga mkono mgombea urais wa CCM, kutokana na kutofuata kanuni na sheria za uchaguzi.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, hivi karibuni alisema waliwaambia TLP na UDP suala hilo lina utaratibu ambao walitakiwa kuufuata, na walipoona hawajafuata, vyama hivyo vimekaa kimya na havisikiki tena.

Aliongeza kuwa UDP waliendelea na kazi zao za kampeni, wakiwa na mgombea wao na kutangaza sera za chama chao. Vile vile, alisema TLP ambao waliweka mabango wameyatoa na wanaendelea na kampeni zao.

IPPMEDIA
 
Msajili anavunja katiba.

Chama chochote kina haki ya kikatiba ya kumuunga mkono mgombea yeyote wakati wowote.

Sheria yoyote itakayokataza hilo inapingana na katiba na hivyo ni batili.

Mimi si mfuasi wa chama chochote. Si mshabiki wa Magufuli.

Napenda haki na kufuata katiba tu.
 
Msajili anavunja katiba.

Chama chochote kina haki ya kikatiba ya kumuunga mkono mgombea yeyote wakati wowote....
Kuna kanuni pia ziliandaliwa kutoka kwenye Katiba, na si kufuata Katiba in general
 
CHAMA cha Tanzania Labor Party (TLP), kimeibuka na kusema kuwa bado kina nia ya kumuunga mkono mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao...
Uhuni wa vyombo vya serekali chini ya awamu hii ni wa viwango vya Jupiter huko!
 
Kuna kanuni pia ziliandaliwa kutoka kwenye Katiba, na si kufuata Katiba in general
Usiwe unajibujibu vitu usivyovifahamu.

Kanuni hazitungwi kutoka kwenye katiba isipokuwa kwenye sheria.

Na kamwe sheria haiwezi kuwa juu ya katiba na pale sheria yeyote inapokinzana na katiba sheria hiyo Ni batili
 
Hahah sa itakuwaje juu ya majibu ya NEC!? Kilicho halali kwa TLP kuwe halali kwa ACT na CDM vyote ni vyama vya siasa.
 
Sasa Tlp hawataitisha
Sheria hii inawahusu ACT only?
 
Safi sana Tlp, lila mtu au chama kina haki ya kumuunga mkono wamtakaye..
 
Back
Top Bottom