Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
TLS-Chama cha Mawakili wa Tanganyika , -Zanzibar wana Chakwao, kimekuwa kikipoteza mvuto na haiba mbele ya jamii kila uchao.
Sababu zinazosemekana kupoteza mvuto kwa jamii:
Sababu zinazosemekana kupoteza mvuto kwa jamii:
- baada ya Uongozi wa Fatuma Karume na Tundu Lissu kumalizika , TLS iliuawa, Edward Hosea na Sungusia ni kama walikuwa Mamluki waliokuja kukiua hicho chama cha Wanasheria, sijui kwanini waliamua kukiua.
- TLS kukaa kimya uminyaji wa haki za binadamu, mawakili kupewa kesi na kuruhusu mahakam, vyama na mashirika kutoa huduma za kisheria tena kwa kuweka matangazo mitandaoni na kwenye Tv huku mawakili wakinyimwa, hiyo mtu anaweka tangazo pale salender bridge kuwa anasajili kampuni kwa laki tatu na wakili anasajili kwa 1.5 m , mteja aende kwa nani?
- Mawakili kuwekwa lupango kama wauza magendo bila sababu na wawekaji kutowajibishwa, na wakili akionekana anaenda kwenye mahojiano huwa wanacheleweshwa ili wakate yamaa na kumuacha mteja.
- Ada za TLS kuwa juu na tuhuma za rushwa ambazo kwenye mikutano ya mawakili kutopatiwa majibu na wanao hoji kuonekana wametumwa na chama cha siasa.
- DAFT- mawakili wanakufa na ugonjwa, njaa ila hakuna mkono wa TLS ila akifa na kuzikwa ndugu wanapewa milioni 6.
- Uchaguzi wa TLS president kukosa mvuto kwa 95% na sasa huenda ukawa kama wa chama cha waendesha mikokoteni.
- Kuamishwa kwa mikutano ya TLS toka Arusha kwenda DODOMA MWAKA 2024. Wasichojua TLs ni kuwa watu wengi , wanakwenda Arusha as adventure, wanakwenda kutalii na kupumzika kwenye hoteli za kitalii na kutembele mbuga za wanyama, kula mbuzi kwa mromboo na mambo mengine mengi. Mawakili wa serikali ambao wameanzisha chama chao kipindi cha JIWE ili TLS ikose nguvu hata wao japo si wanachama wa TLS lakini huwa wanakwenda mikutano ya TLS maana wanaipenda TLS KULIKO CHAMA CHAO .Huko Dodoma hawatakwenda, kutadoda.
- Kamati ya maadili ya mawakili imekuwa kama kisu kwa mawakili, yani huko badala member atetewe wao ndio kwanza wanamfungia, mfano Shangazi Fetty na wengine wengi. Kila chama, kuanzia cha majaji, mahakimu, walimu, madereva , umoja wa madereva bodaboda, wanatetea haki zao na wana wivu kweli na mwanachama wao ila TLS wao wanaangamiza wanachama wao!
Bali sasa Ujio wa Boniface Mwabukusi kwenye uongozi wa Chama hicho ni sawa na Ufufuo na Uzima, japo huenda akaenguliwa, kuna siasa nyingi .