TLS Kuunda kamati Maalum Sakata la Ngorongoro

TLS Kuunda kamati Maalum Sakata la Ngorongoro

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi amesema Baraza la Uongozi la chama hicho limeunda kamati maalum kufuatilia suala la Ngorongoro ili kujua ukweli wake

Mwabukusi amezungumza hayo alipokutana na wanahabari leo, Jumanne Agosti 20.2024 ambapo amesema pamoja na kufuatilia suala hilo kamati hiyo litafanya kazi zifuatazo;

(I) Kufanya mashauriano na taasisi mbalimbali pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo yenye migogoro ili kujua uhalisia wa migogoro husika

(ii) Kufanya mapitio ya sera, sheria na mazoea pamoja na kuzichambua kuhusiana na umiliki wa ardhi kwa wazawa pamoja na shughuli za uwekezaji na uhifadhi na kubaini uzingativu wa haki za msingi za raia katika maeneo husika kwa kuzingatia Katiba, sera na sheria za nchi

(iii) Kuandaa kongamano (Symposium) la kitaifa kuhusiana na namna bora ya kufanya maendeleo kwa kuzingatia na kulinda haki za wazawa katika ardhi zao za asili pamoja na haki zao za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni katika maeneo yanayofikiwa na shughuli za uwekezaji.
Chanzo .mwanzo Tv
 
Back
Top Bottom