TLS waendesha Mjadala wa Wazi Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya Tanzania

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Fatilia mjadala wa wazi wa wadau uliyo andaliwa na chama cha wanasheria Tanzania bara (TLS) kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya Tanzania.

Je, ni lini katiba mpya itapatikana Tanzania?.

RECORED🎥 (01/06/2024)👇

View: https://www.youtube.com/live/1mqjtzRdvN4?si=r9LuZeIFoyzjlD-d

RECORDED 🎥 (25/05/2024)👇

View: https://www.youtube.com/live/ZSwhE8mIzHI?si=4oelwWdeO4LfCvjw[/URL]

Muendelezo wa mjadala huu unaendelea kupitia katika Threads: Mjadala wa Wazi Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya Arusha.
 
Ccm ndio hawataki katiba mpya Kwasababu katiba iliyopo ina maslai kwao.
Binafsi naona hata sisi wananchi tunachangia kuchelewesha mchakato wa katiba mpya, ingawa hili linachangiwa na mfumo uliowekwa na serikali. Nitafafanua✍️.

Serikali imeweka mfumo mbovu kwa Watanzania kupata maarifa kuhusu masuala ya sheria. Mfumo huu unalazimisha Mtanzania kufikia ngazi ya chuo kikuu na kusomea masomo ya sheria (LL.B) ili kujua mambo muhimu ya kisheria.

Matokeo yake, Watanzania wengi wamejitenga kabisa na masuala ya kisheria. Kumbuka, katiba ni sheria mama. Hivi sasa, tunaishi katika taifa ambalo zaidi ya 90% ya wananchi hawana uelewa wa katiba, lakini zaidi ya 80% wanataka katiba mpya. Cha kushangaza, kati ya hawa 80%, ni 10% tu wanaojua na kuelewa katiba. Hali inakuwa mbaya zaidi mtu anaposema anataka katiba mpya lakini hawezi kueleza ni ibara gani anataka irekebishwe. Je, watu wa namna hii wanaweza kuwa na hoja za msingi za kuishawishi serikali ya kukubali kubadili katiba🤔? Jibu ni HAPANA.

Nilifurahishwa na kauli ya mama miezi minane iliyopita kwamba lazima wananchi wafundishwe katiba kwanza kabla ya kuirekebisha, kwa maana katiba ni mali yao (ingawa suala hili linachelewa kwa kiasi fulani). Kwa upande mwingine wa shilingi, nadhani serikali inatakiwa kupitia upya sera za elimu na kuanzisha moduli za masuala ya sheria kuanzia ngazi ya shule ya msingi.

Mwisho, ili kuhakikisha mchakato wa katiba mpya unafanikiwa, ni muhimu kwa wananchi kuwa na uelewa mzuri wa katiba na masuala ya kisheria kwa ujumla. Hili litasaidia kuwa na mjadala wenye tija na hoja za msingi zitakazosaidia kuboresha katiba yetu.

View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=XUj7KNwsLjtLjw7v
 
🙌🙌🙌Upewe nchi
 
Mods Active na wengine. Naomba Prefix ya LIVE kwa muda katika mjadala huu🙏. Maana mjadala unaendelea na leo.​
 
Back
Top Bottom