SeriaJr TW
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 246
- 224
Chama cha mawakili Tanganyika (TLS) kimepata pigo baada ya aliyekuwa mwanachama cha Chama hicho wakili Loomu Ojare kufariki dunia ghafla akiwa kazini.
Ojare alifariki dunia na kuzikwa nyumbanj kwake mapema skku kadhaa zilizopita baada ya kuugua ghafla akiwa kazini na hivyo kuacha pengo kubwa katika tasnia ya sheria.
Mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea Kanda ya Arusha Elibariki Maeda akiiwakilisha TLS katika ibada ya kumuaga Ojare alisema kifo cha Ojare ni pigo kwa Chama na wanachama wa chama hicho kwa kuwa alikuwa akishirikiana vizuri na mawakili wenzake
Ojare alizaliwa mwaka 1953 na alifanya kazi kama mwanasheria wa serikali katika maeneo mbalimbali ambapo mwaka 1983 alianza kufanya kazi kama wakili wa kujitegemea hadi umauti unamkuta.