TLS ya Mwabukusi: Anza na Haya: Majaji Wanaoharibu Kesi na Ucheleweshaji wa Kusikiliza

TLS ya Mwabukusi: Anza na Haya: Majaji Wanaoharibu Kesi na Ucheleweshaji wa Kusikiliza

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
1.0 Kuanzia Mahakama za chini hadi Mahakama Kuu suala la Hakimu au Jaji kuharibu kesi kwa manufaa yake ni la kawaida tu. HAWAJALI.

Wanajificha kwenye mstari wa mwisho wa hukumu zao unaosema "mlalamikaji/ mlalamikiwa ana haki ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya juu"

Mfumo wa kutengeneza rufaa Tanzania siyo kitu chepesi kwa kuwa huchukua muda mwingine na raslimali fedha. Kitendo cha kuchelewesha haki nako ni kunyima haki.

Pendekezo:
Itungwe sheria ambayo Judicial Service Commission ikiridhika kuwa Jaji/ Hakimu alitoa hukumu chini ya kiwango kwa sababu za uzembe na corruption basi ACHUKULIWE hatua za Kinidhamu.

2.1 Ni kawaida kuazia Mahakama za chini hadi Mahakama Kuu kesi inaweza ikaahirishwa hata miezi 9 au mwaka mzima bila kusikilizwa. Kila siku ikipangwa utasikia sababu tofauti za kuahirisha.

Pendekezo
Itengemezwe sheria itakayowabana Mahakimu/ Majaji kutoa hukumu kwa muda maalum. Ikithibitika ni uzembe basi hatua zichukuliwe dhidi ya mhusika

3. Mahakama ya Rufaa kwa mwezi huu wa Agosti 2024 inasilkiliza mashauri ya mwaka 2019- 2021 na baadhi za 2022. Sasa za mwaka 2023 na 2024 sijui zitasikilizwa lini.

Pendekezo:
Majaji wa Rufaa waongezwe, lakini pia na idadi ya sessions wanazofanya ziongezwe pia.
 
Bila shaka liko juu ya uwezo wake
Kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya TLS sura ya 307 kifungu (c) na (d) malengo ya kuanzishwa TLS ni:

(c) Kuisaidia serikali na mahakama katika mambo yote yanayohusu sheria, utawala wa sheria na utekelezaji wa sheria;

(d) Kulinda na kuusaidia umma wa watanzania yanayohusu au kuendana au kutokana na sheria;

Je hizo hoja kwenye mada unaona hazikidhi kwenye sheria ya TLS? AU mnataka Mwabukusi akafanye HARAKATI?
 
Back
Top Bottom