TLS yamchamba Ndumbaro, yasema inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni na haijawahi kukurupuka kwenye matamko yake

TLS yamchamba Ndumbaro, yasema inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni na haijawahi kukurupuka kwenye matamko yake

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
TLS [Chama cha Wanasheria Tanganyika] kikiongozwa na rais wake Machachari Boniface Anyunywile Mwabukusi kimetoa tamko ambalo kwa vijana wa kijani wanaona kama ni kuchamana na Ndumbaro.

chama hicho kimeelezea kusikitihwa na kitendo cha Ndumbaro ambaye ni waziri wa sheria kukabishi gari la msaada tena kutoka kwa wahisani LEGAL SECTOR REFORM PROGRAM [LSRP]kuwataka kutotoa matamko dhidi ya ukandamizaji wowote.

Ikumbukwe, Ndumbaro ni Wakili mwenye Kampuni iitwayo MELETA AND NDUMBARO ADVOCATES inayofanya shughuli zake Dar es salaam lakini hawa hawa mawakili ndio kama wanangusha sekta ya Sheria.

KWA KIFUPI TLS imeonyesha namna ambavyo hata Ndumbaro alivyo mweupe kichwani na hajui:

Soma Pia: Waziri Ndumbaro: Serikali haipendi kabisa matamko ya kukurupuka ya TLS

  1. TLS imeanzishwa na Sheria ya Bunge, Sura No. 307 na Majukumu yake yapo ibara ya 4 ya sheria hiyo.
  2. Tangu kuanzishwa kwa TLS imekuwa ikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake. Mfano TLS ilipinga wananchi kuondoshwa Ngorongoro na serikali ikatii
  3. Matamko ya TLS yanatolewa kwa mujibu wa kifungu cha nne cha sheria ya TLS.
  4. TLS imepewa gari, gari
  5. limesajiliwa na SErikali, namba ni STN, mali ya Wizara ya Sheria na Katiba na limetolwa msada na LEGAL SECTOR REFORM PROGRAM.
  6. TLS imemtaka ndumbaro anedelee kushirikana nao.
#Je, ni kweli TLS imeufyata?

vvvvv.jpeg

======

Screenshot 2024-12-17 194215.png
Screenshot 2024-12-17 194240.png
 
Mwabukusi ninayemjua angekiwasha, sasa sijui kaingia hofu, au hataki kuongea wakati wa kula, atafanya vipande vya wali na kuku virukie wakubwa kutoka mdomoni mwake.

Ni kama anasema "nimekosa mini, nimekosa sana.

=====================

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Mhe. Dr. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria siku ya tarehe 16 Desemba, 2024 wakati wa kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya TLS na Wizara ambapo, miongoni mwa mambo mengine, Mhe. Waziri alinukuliwa akisema "kama kuna kitu ambacho serikali haipendi kabisa ni yale matamko ya kukurupuka kutoka TLS".

Soma Pia: Waziri Ndumbaro: Serikali haipendi kabisa matamko ya kukurupuka ya TLS

Screenshot 2024-12-17 194215.png

Screenshot 2024-12-17 194240.png
 
Attachments

Truth be told ni kweli tunakurupuka sana nyakati hizi.

Ila ulichokandika mleta uzi ni tofauti na kilichotolewa.
 
Mwabukusi na Ndumbaro wote ..wale wale wa OUT....wanajuanaaa haoo
 
On the same page

TLS ni chama kama ilivyo vingine kama ERB, TANNA, MCT, MAT etc

Waache kuburuza agenda zisizo na maana kwa taifa... Na hata hili tamko ni la kukurupuka...

You cant eat your cake and have it...
Apande Landcruiser hiyo STN ale maisha😂
 
Mwabukusi aache hizi mbio, afate Muongoza wa chama. Yuko very short tempered. Alafu mlengo wake si mzuri na chama.. aache hili mara moja.
 
Huyo waziri kakalia kuti kavu.....
Mama anaweza kumbinua, alitakiwa aongee kidiplomasia, TLS wamemuheshimu, angewaheshimu, hasa season hii mama anapokuwa anasoma kitabu cha jinsi ya kupata ushindi 2025,hataki kelele za mtu, au asababishiwe kelele na mtu
 
..Waziri Ndumbaru ni m-pu-mbavu.

..hakutakiwa kutoa kauli za VITISHO kwa chama cha wanasheria.
 
TLS [Chama cha Wanasheria Tanganyika] kikiongozwa na rais wake Machachari Boniface Anyunywile Mwabukusi kimetoa tamko ambalo kwa vijana wa kijani wanaona kama ni kuchamana na Ndumbaro.

chama hicho kimeelezea kusikitihwa na kitendo cha Ndumbaro ambaye ni waziri wa sheria kukabishi gari la msaada tena kutoka kwa wahisani LEGAL SECTOR REFORM PROGRAM kuwataka kutotoa matamko dhidi ya ukandamizaji wowote.

Ikumbukwe, Ndumbaro ni Wakili mwenye Kampuni iitwayo MELETA AND NDUMBARO ADVOCATES inayofanya shughuli zake Dar es salaam lakini hawa hawa mawakili ndio kama wanangusha sekta ya Sheria.

KWA KIFUPI TLS imeonyesha namna ambavyo hata Ndumbaro alivyo mweupe kichwani na hajui:

Soma Pia: Waziri Ndumbaro: Serikali haipendi kabisa matamko ya kukurupuka ya TLS
  1. TLS imeanzishwa na Sheria ya Bunge, Sura No. 307 na Majukumu yake yapo ibara ya 4 ya sheria hiyo.
  2. Tangu kuanzishwa kwa TLS imekuwa ikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake. Mfano TLS ilipinga wananchi kuondoshwa Ngorongoro na serikali ikatii
  3. Matamko ya TLS yanatolewa kwa mujibu wa kifungu cha nne cha sheria ya TLS.
  4. TLS imepewa gari, gari
  5. limesajiliwa na SErikali, namba ni STN, mali ya Wizara ya Sheria na Katiba na limetolwa msada na LEGAL SECTOR REFORM PROGRAM.
  6. TLS imemtaka ndumbaro anedelee kushirikana nao.
#Je, ni kweli TLS imeufyata?

View attachment 3178994

======

Hao washafungwa speed governor.
Hayo maneno sio mageni hapa jijini.
 
Andika taratibu basi mkuu

Hao washafungwa speed governor.
Hayo maneno sio mageni hapa jijini.
Kwahiyo , wewe kama mwanaharakati huru, ungependa TLS ikatae gari la serikali ?
Mwabukusi ni rais wa TLS na ana ofisi zake Mbeya na Rais hakai ofisini isipokuwa CEO ndio anakaa ofisini , je Rais akatae gri wakati hata CEO anahitaji?
TLS ipinge kila kitu hata kama ni halali?
 
Umeniquote hapo, ulikusudia kumuuliza nani swali Hilo?
 
Kuna mahali taarifa imetolewa kwamba Mwabukusi amekabidhiwa gari kama Zawadi na serikali! Au ni TLS imepewa gari! Fikra tunduizi
Imeshafafanuliwa kule X kuwa huyo alionekana kwenye picha sio Mwabukusi bali tu anafanana naye
 
Back
Top Bottom