Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda tume maalumu ya kuchunguza ushiriki wa Jeshi la Polisi kwenye masuala ya utekaji na utesaji kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likituhumiwa kushiriki katika vitendo hivyo.
Kupitia taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa Agosti 09, 2024 na Baraza la Uongozi la TLS na kusainiwa na Rais wake Boniface Mwabukusi, TLS imeeleza kusikitishwa na kulaani vitendo vya kukamatwa, kutekwa na kuteswa kiholela kwa wananchi kunakoendelea nchini bila ya vyombo husika vya dola “kuwajibika ipasavyo”.
“Mara kwa mara Jeshi la Polisi limekuwa likikanusha kutokea kwa matukio hayo lakini baadaye inakuja kubainika kwamba matukio hayo ni ya kweli. Mara nyingine Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata raia wema wanaotoa taarifa hizo kwa kile kinachosemekana kusambaza taarifa za uongo badala ya kufanyia kazi taarifa hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria”, ameeleza Mwabukusi.
TLS imeeleza pia kuwa hakuna taarifa kamili ya uchunguzi wa tukio hata moja ambayo imewahi kutolewa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi juu ya watuhumiwa wa matukio hayo na kwamba hali hiyo imeendelea kutia hofu wananchi juu ya usalama wao na mashaka juu ya uwezo wa Jeshi la Polisi kuchunguza na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wa matukio hayo.
Katika kujaribu kutatua changamoto za matukio hayo nchini, TLS pia imependekeza kuundwa kwa chombo maalumu cha kudumu cha kuangalia utendaji wa vyombo vya dola (oversight body) ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa mujibu wa Katiba na Sheria huku ikilitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi yake kwa weledi ili kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi na mali zao unaimarika.
Katika taarifa ya TLS kumeorodheshwa matukio mbalimbali ya utekaji yaliyoripotiwa na vyombo vya habari na watu mbalimbali likiwamo tukio la karibuni la Kombo Mbwana aliyetekwa nyumbani kwake Handeni Tanga na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 15 Juni 2024, baadaye polisi walikanusha kuhusika na kufungua jalada la uchunguzi, na Siku 29 baadaye polisi walikiri kuhusika na kumshikilia kwa hizo siku zote.