Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) kikiongozwa na wakili Boniface A.K Mwabukusi kimetoa tamko zito lililoweka wazi hali ya kusikitisha inayolikumba taifa. Kwa mujibu wa tamko hilo, kumekuwa na ongezeko la matukio ya kutekwa, kupotea, na kuteswa kwa watu nchini Tanzania, huku vyombo vya dola vikishindwa kutoa ufafanuzi wa kuridhisha au kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo hivi vya kikatili.
TLS imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu jinsi Jeshi la Polisi limekuwa likishughulikia matukio haya. Licha ya taarifa nyingi kutolewa kuhusu utekaji na utesaji, mara kwa mara vyombo hivi vimeonekana kukanusha madai haya, hata pale ambapo ushahidi wa kutosha umeibuka kuthibitisha ukweli wa matukio haya. Hali hii imeongeza hofu na wasiwasi miongoni mwa wananchi, ambao wanahisi kutokuwa salama katika nchi yao wenyewe.
Katika tamko hilo, TLS inakemea vikali vitendo vya utekaji na utesaji, ikieleza kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kama ilivyowekwa bayana katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mikataba ya kimataifa. TLS imeishauri serikali, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kuchukua hatua za haraka kuunda Tume Maalum itakayochunguza matukio haya na kubaini wahusika wa uhalifu huu.
Aidha, chama hicho kinapendekeza kuanzishwa kwa chombo maalum cha kudumu kitakachokuwa na jukumu la kusimamia na kuangalia utendaji wa vyombo vya dola, kuhakikisha vinafanya kazi kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Kwa kufanya hivyo, TLS inaamini kuwa itaimarisha uadilifu wa vyombo vya dola na kurejesha imani ya wananchi kwa serikali yao.
Katika kiambatanisho cha tamko hilo, TLS imetoa orodha ya baadhi ya watu waliotekwa au kupotea kuanzia mwaka 2016 hadi 2024, ikiwa ni ushahidi wa dhahiri wa kuendelea kwa vitendo hivi vya kikatili. Baadhi ya watu hao walipatikana wakiwa wamejeruhiwa, huku wengine wakiwa hawajulikani walipo hadi sasa.
Kwa kuhitimisha, TLS inatoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari za ziada katika maisha yao ya kila siku, na kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo watahisi hatari yoyote. Huu ni wakati muhimu kwa Watanzania wote kusimama pamoja katika kupinga vitendo hivi vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kudai uwajibikaji kutoka kwa viongozi.
Pia soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
TAMKO 👇🏼

09 Agosti, 2024
TAARIFA KWA UMMA
ONGEZEKO LA VITENDO VYA UTEKAJI NA UPOTEAJI WA WATU NCHINI
ONGEZEKO LA VITENDO VYA UTEKAJI NA UPOTEAJI WA WATU NCHINI
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinasikitishwa na kinalaani vitendo vya kukamatwa, kutekwa na kuteswa kiholela kwa wananchi kunakoendelea nchini bila ya vyombo husika vya dola kuwajibika ipasavyo.
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za watu kupotea katika mazingira tatanishi, kutekwa na kuteswa na baadae kuonekana huku baadhi yao wakiwa wamefariki na wengine wakiwa na majeraha makubwa katika miili yao. Tunasikitishwa pia na namna ambavyo vyombo vyetu vya dola hususani Jeshi la Polisi limekuwa likifanyia kazi taarifa hizo. Mara kwa mara Jeshi la Polisi limekuwa likikanusha kutokea kwa matukio hayo lakini baadae inakuja kubainika kwamba matukio hayo ni ya kweli. Mara nyingine Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata raia wema wanaotoa taarifa hizo kwa kile kinachosemekana kusambaza taarifa za uongo badala ya kufanyia kazi taarifa hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zinazowapasa kufanya wajibu wao wa kulinda watu na mali zao.
TLS, kwa mamlaka iliyopewa kupitia kifungu cha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002), inapenda kuvikumbusha vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi juu ya majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria ya kulinda watu na mali zao. Matukio haya ya utekaji ni kinyume na Ibara ya 13 (6) (e) na 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; pamoja na Mikataba ya Kimataifa inayozungumzia Haki za Binadamu na inayozuia uteswaji wa watu kama vile Mkataba dhidi ya Mateso na Unyanyasaji au Adhabu Nyingine za Kikatili au Udhalilishaji (Convention against Torture and Other Cruel, Inhuman or Degrading Treatment or Punishment), Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (The International Covenant on Civil and Political Rights).
TLS inatambua na kuheshimu taarifa za Jeshi la Polisi zinatolewa zikitaarifu umma kwamba matukio hayo yamekuwa yanafanyiwa uchunguzi lakini tunasikitika kwamba hakuna taarifa kamili ya uchunguzi wa tukio hata moja ambayo imewahi kutolewa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi juu ya watuhumiwa wa matukio hayo. Hali hii inaendelea kutia hofu kwa wananachi juu ya usalama wao na mashaka juu ya uwezo wa Jeshi la Polisi kuchunguza na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wa matukio hayo.
Kupitia tamko hili, tunaambatanisha orodha ya baadhi ya watu ambao wananchi au/na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimewahi kutoa taarifa za kupotea au kutekwa kwao ambapo baadhi yao walipatikana na baadhi yao wakiwa na majeraha huku kukiwa na wengine ambao waliopotea katika mazingira tatanishi na hawajapatikana mpaka leo. Tunaamini kwamba Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola vitafanyia kazi na kuhakikisha watu hao wamepatikana na wahusika wote wa matukio haya wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo husika vya haki ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Wito wetu;
- Tunamshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume maalumu ya kuchunguza matukio yote ya kupotea kwa watu, kutekwa na kuteswa;
- Tunamshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda Tume Maalum ya kuchunguza ushiriki wa Jeshi la Polisi kwenye masuala ya Utekaji kwa kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likituhumiwa kushiriki katika vitendo hivyo;
- Tunapendekeza kuundwa kwa chombo maalumu cha kudumu cha kuangalia utendaji wa vyombo vya dola (oversight body) ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa mujibu wa Katiba na Sheria; na
- Tunalitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi yake kwa weledi kwa mujibu wa Katiba na Sheria ili kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi na mali zao unaimarika
TLS inaendelea kufuatilia matukio haya kwa ukaribu na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya dola katika kuhakikisha wahusika wote wa matukio haya wanafikishwa katika vyombo mahususi vya haki ili haki ionekane inatendeka. Hata hivyo, tunatoa rai kwa watanzania wote kuwa makini wakati wote na kutokubali kuitwa au kukutana na watu wasiowajua au kwenda mahali wasipopajua na ikibidi sana wawasiliane na wakili yeyote kabla ya kukutana au kwenda mahali wasipopajua.
Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Boniface A.K Mwabukusi
Rais
Boniface A.K Mwabukusi
Rais
KIAMBATISHO:
ORODHA YA WATU WALIOTEKWA/KUPOTEA 2016-2024.
| S/N | JINA | MAELEZO MAFUPI | MAKAZI |
| 1. | KOMBO MBWANA TWAHA | Alitekwa nyumbani kwake Handeni Tanga na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 15 Juni 2024, baadaye polisi walikanusha kuhusika na kufungua jalada la uchunguzi. Siku 29 baadaye polisi walikiri kuhusika na kumshikilia kwa hizo siku zote. | Handeni - Tanga |
| 2 | KENNEDY MWAMLIMA | Alitekwa Mbeya na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 11 Aprili 2024. Alipatikana Igunga Tabora Tarehe 16 Aprili 2024 akiwa ametapakaa majeraha. Kwa maelezo yake alikuwa akiteswa katika vituo vya polisi na alikuwa akiulizwa nani anamtuma kukosoa serikali katika mtandao wa TikTok. | Mbeya Jiji -Mbeya |
| 3 | EDGER MWAKALEBELA | Alitekwa tarehe 23 Juni 2024 Ubungo Dar es Salaam. Akapelekwa kituo cha polisi Arusha kabla ya kupatikana tarehe 27 Juni 2024 mkoani Katavi porini akiwa ametapakaa majeraha.OysterBay na baadaye | Dar es Salaam. |
| 4 | JAMES SIJE | Alitekwa na askari polisi anayeitwa Sgt. Mageni Musobi A.K.A Majani wa kituo cha polisi Nyakato tarehe 17 Agosti 2021 mpaka sasa hajapatikana. | Nyakato –Mwanza |
| 5 | JOSEPH MNYONGA | Alitekwa Julai 2021 nyumbani kwake Mwanza na watu waliojitambulisha kuwa | Mwanza. |
ni askari polisi kutoka mkoa wa Mwanza mpaka sasa hajapatikana. | ||||
| 6 | DOTTO KABWA | Alitekwa tarehe 4 Julai 2022 na askari polisi anayejulikana kwa jina la Wambura Mwita kutoka kituo cha polisi Ifunda Iringa na hajapatikana mpaka leo. | Ifunga-Iringa | |
| 7 | YAHYA ALLY | Alitekwa tarehe 6Septemba 2022 Mbagala Kizuiani na askari polisi wakiongozwa na OC-CID Abdalah Suleiman. Mpaka sasa hajapatikana. | Mbagala – Dar es Salaam. | |
| 8 | CHANDE KIZEGA | Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 18 Agosti 2022 akiwa dukani kwake Machinga Complex. Mpaka sasa hajapatikana. | Dar es Salaam | |
| 9 | Mzee SAMUEL MKONGO | MATIKO | Alitekwa mkoani Geita tarehe 27 Januari 2023 na askari polisi Sgt. Hamis mwenye namba 0789938835 na kupelekwa kituo cha Muriaza –Butiama mkoani Mara. Ndugu walifika hapo na wakamuona akiwa ametapakaa majeraha, lakini waliporudi kumletea chakula hawakumkuta tena kituoni hapo na hajaonekana mpaka leo. | Geita mjini. |
| 10 | CHARLES MWAMPYATE | ADEN | Alitoweka tangu tarehe 7 Decemba 2023 akiwa Dar es Salaam na hajapatikana mpaka leo. | Dar es Salaam. |
| 11 | WILLIAM HERMAN | Alitekwa Mwanza tarehe 1 Januari 2024 na askari polisi anayefahamika kwa jina la Sgt. Mageni Musobi A.K.A | Kangaye-Mwanza |
Majani wa kituo cha polisi Nyakato. | |||
| 12 | DAVID GASPER LEMA | Alipotea akiwa njiani kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam tangu tarehe 6 Aprili 2024 na mpaka sasa hajapatikana. | Mwanza |
| 13 | JEROME KISOKA a.k.a MAPII | Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 14 Novemba 2023 eneo la Njoro, Moshi mkoani Kilimanjaro na hajapatikana mpaka leo. | Moshi-Kilimanjaro |
| 14 | RIDHIWANI HEMED MSANGI (PIA AMEKUWA AKIJULIKANA KWA JINA LA ABDALLAH SALUM MSANGI) | Alipotea mkaoni Iringa mwishoni mwa mwezi Julai 2021 na hajapatikana mpaka leo. Kazi yake alikuwa mhadhiri (Lecturer) Chuo Kikuu cha Mkwawa ambalo ni tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. | Iringa |
| 15 | BENSON E.A. ISHUNGISA | Alitekwa na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 26 Novemba 2023 akiwa nje ya Hospital ya Makangarawe Yombo mkoani Dar es Salaam. Benson alikuwa akimsubiri abiria nje ya Hospital hiyo na hata bodaboda wenzake walipoulizwa kituo cha polisi anachopelekwa hawakujibiwa. Mpaka leo hajapatikana. | Dar es Salaam |
| 16 | HAMZA SAID | Katibu wa chama cha NCCR Mageuzi mkoa wa Geita. Alitekwa tarehe 17 Decemba 2023 nyumbani kwake mtaa wa Mwatulole mkoani Geita na watu waliojitambulisha ni askari polisi. Mpaka leo Katibu huyo hajapatikana | Mwatulole-Geita |
| 17 | YONZO SHIMBI DUTU | Alikamatwa tarehe 2 Machi 2024 na askari polisi wa kituo cha polisi Kwimba Mwanza akiwa na wenzake maeneo ya Bushini-Kishapu mkoani Shinyanga. Wenzake waliachiwa ila yeye hajapatikana na hayupo vituo vyote vya polisi. | Kishapu-Shinyanga |
| 18 | LILENGA ISAYA LILENGA | Alitekwa tarehe 11 Mei 2024 maeneo ya Kibirizi mkoani Kigoma na watu wanaodaiwa ni polisi kisha kutokomea naye kusikojulikana. Mpaka sasa hajapatikana. | Mwandiga-Kigoma |
| 19 | TAWAFIQ MOHAMED | Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana. | Dar es Salaam |
| 20 | SELF SWALA | Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana. | Dar es Salaam |
| 21 | EDWIN KUNAMBI | Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana. | Dar es Salaam |
| 22 | HEMED ABASS | Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es | Dar es Salaam |
| Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana. | |||
| 23 | RAJABU MDOE | Alitekwa tarehe 26 Decemba 2021 eneo la Kamata, Kariakoo mkoani Dar es Salaam akiwa na wezake wanne. Watekaji walijitambulisha kuwa ni askari polisi na mpaka sasa hajapatikana. | Dar es Salaam |
| 24 | MZEE HAJI SOFT | Alichukuliwa nyumbani kwake Temeke na watu waliojitambulisha ni askari polisi tarehe 13 Julai 2021 na mpaka sasa hajapatikana. | Temeke – Dar es Salaam |
| 25 | ALPHONCE BILASENGE | Alitoweka ghafla. Simu yake mara ya mwisho ilizimwa eneo la Kibeta, wilaya ya Bukoba mjini mkoani Kagera tarehe 6 Januari 2022. | Kagera |
| 26 | ALBERT KISEYA SELEMBO | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi akiwa na kesi ya Mauwaji. | Loliondo - Arusha |
| 27 | MOLOIMETI YOHANA SAING’EU | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha Polisi akiwa na kesi ya Mauwaji. | Loliondo - Arusha |
| 28 | NDIRANGO SENGE LAIZER | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 | Loliondo - Arusha |
| wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | |||
| 29 | JOEL CREMES LESSONU | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 30 | SIMONI NAIRIAM OROSIKIRIA | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 31 | DAMIAN LAGO LAIZER | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 32 | MATHEW ELIAKIMU SILOMA | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 33 | LUKAS K. NJAUSI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 34 | TALENG’O TWAMBEI LESHOKO | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 35 | KIJOOLU KAKEI OLOJILOJI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo – Arusha |
| 36 | SHENGENA JOSEPH KILLEL | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 9 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo Arusha |
| 37 | MASEKE MWITA MASEKE | Alitoweka tangu tarehe 10 Juni 2022 mpaka sasa hajapatikana. | Nkerege -Tarime- Mara |
| 38 | MALONGO DANIEL PASCHAL | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya | Loliondo - arusha |
| serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | |||
| 39 | SIMELI PARMWATI KARONGOI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 40 | INGOI OLKEDENYI KANJWEI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 41 | SANGAU MORONGETI NGIMINIS | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 42 | MARIJOI NGOISA PARMATI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 43 | MORONGETI MASAKO | MSEEKI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 44 | KAMBATAI LULU | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha | |
| 45 | ORIAS OLENG’IYO | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 10 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo -Arusha | |
| 46 | WILSON KOLONG | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 12 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha | |
| 47 | JAMES TAKI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 13 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye | Loliondo - Arusha |
| aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | |||
| 48 | JOSEPH JARTAN | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 13 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 49 | KELVIN SHASO NAIROTI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 15 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 50 | LEKERENGA KOYEE ORODO | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 15 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo -Arusha |
| 51 | FRED VICTOR LEDIDI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 15 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | Loliondo - Arusha |
| 52 | SIMON MORINTANTI | Alitekwa na watu wenye silaha tarehe 15 Juni 2022 wakati wa oparesheni ya serikali kuhamisha watu kwa | Loliondo - Arusha |
| nguvu huko Loliondo. Baada ya wiki tatu alipatikana kituo cha polisi na baadaye aliachiwa baada ya mashtaka dhidi yake kukosa ushahidi. | |||
| 53 | MOHAMED KAYEGO KALEBE | Alikamatwa na watu wengine sita (6) na maafisa waliojitambulisha kuwa ni askari polisi tarehe 5 Apriil 2023 huko Katoro mkoani Geita. Ndugu walifika vituo vyote vya polisi hawakumkuta na hajapatikana mpaka leo yeye na hao wenzake ambao majina hayajatambulika mpaka sasa. | Katoro - Geita |
| 54 | AMON MRIGI MAGIGE | Alikamatwa na askari wa jeshi la Polisi wakiwa na gari za Polisi Land Cruiser Pick Up mbili hapo tarehe 1 Octoba 2023. Mpaka sasa hajapatikana na hayupo kituo chochote cha polisi wala gerezani. | Mwanza |
| 55 | AZIZ KINYONGA | Alipotea siku kadhaa, kwa maelezo ya mke wake anasema baada ya mume wake kupotea siku kadhaa baadaye ilifika gari aina ya Toyota Noah na ndani ya ile gari alionekana mtu akinyosha kidole kuonyesha nyumba yao. Mke anasema hakujua ni mume wake. Anadai walishuka watu waliojitambulisha ni askari walikagua nyumba wakakuta kuna laki mbili wakachukua na kuondoka. Baadaye gari ya mume wake Aziz lilikutwa limetelekezwa mkoani Mtwara. Hajapatikana tangu tarehe 1 Februari 2023. | Chamazi – Dar es Salaam. |
| 56 | YUSUPH DUDU | Alitekwa nyumbani kwake na watu wenye silaha waliojitambulisha ni polisi. Watu hao walipofika nyumbani kwa Yusuph walimkuta mtoto wake mwenye miaka 8 wakamwambie kamwite baba yako na kisha Yusuph alivyofika walijitambulisha ni askari polisi na kuondoka naye tangu tarehe 9 Aprili 2024 mpaka sasa hajapatikana. Jarada la uchunguzi la kupotea kwake limefunguliwa kituo cha polisi Mbagala Maturubai MBL/RB/2891/2024. | Mbagala – Dar es Salaam |
| 57 | KASTORY KAPINGA | Mwanafunzi wa chuo cha SAUT, kituo cha Arusha mwaka wa tatu alipotea akiwa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma tangu mwanzoni mwa mwezi Aprili 2024. Hajapatikana mpaka sasa. | Ruvuma - Mbinga |
| 58 | DIONIZ KIPANYA | Alitoweka tangu tarehe 27 Julai 2024 huko Sumbawanga mkoani. Hajapatikana mpaka leo. | Sumbawanga- Rukwa |
| 59 | SHADRACK CHAULA | Alitekwa tarehe 2 Agosti 2024 kijijini kwao Ntokela, wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Siku 20 kabla ya kutekwa Shadraka Chaula alitolewa jela kwa michango ya watanzania walioamua kumlipia faini baada ya kufungwa jela au kulipa faini kwa kosa la kuchoma picha ya Rais Samia Suluhu Hassan. | Ntokela – Rungwe – Mbeya |
| 60 | PROSIPER THEONAS MNJARI | Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa Polisi na walikuwa wameongozana na watumishi wa TANESCO. Watekaji wao walisema nyumba yao ina deni kubwa sana la umeme yeye akajibu kuwa ni mpangaji tu awaunganishe na mwenye nyumba lakini walikataa na kuondoka naye mpaka sasa hajapatikana. | Chamazi – Dar es Salaam |
| 61 | THOMAS MUNGO IHUYA | Alikuwa anafanya kazi Mahakama kuu Mwanza alipotea tangu March 2018 mpaka leo hajapatikana. | Mwanza |
| 62 | DENNIS KANTANGA | Alikuwa mkazi wa mkoa wa Shinyanga Mjini na alikuwa akifanya shughuli za TEHAMAkwa maana ya kutengeneza na kuuza computers, desktop pamoja na laptops na vifaa vingine vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo CCTV. Siku anachukuliwa alifuatwa dukani kwake na watu wawili au zaidi lakini waliofika dukani walikuwa wawili na kujitambulisha kuwa ni askari. Waliondoka kwa gari yake mwenyewe(Dennis) na ikawa mwisho wa kusikikika kwake. Katika utaratibu wa kuripoti polisi na kutrack simu ilionekana simu yake iliwashwa wilayani Musoma mkoani Mara na baada ya hapo haikupatikana tena. Gari yake ilikuja kupatikana maeneo ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa imeegeshwa katikati ya mji | Shinyanga |
| baada ya wiki moja. Ni miaka 4 sasa imepita toka kutoweka kwake. | |||
| 63 | Damas Vedastus Bulimbe | Alipotea tarehe 15 Novemba 2023 huko Geita. Hajapatikana mpaka leo. | Geita |
| 64 | Lucas Magambo Bulimbe | Alipotea tarehe 15 Novemba 2023 huko Geita. Hajapatikana mpaka leo. | Geita |
| 65 | Matuki Makuru | Alitoweka tarehe 15 Februari 2024 wilayani Serengeti mkoani mara. Hajapatikana mpaka leo. | Serengeti, Mara |
| 66 | Dastan Gervas Nestory | Alitoweka tarehe 9 Julai 2024 huko Mkoani Geita. Hajapatikana hadi sasa. | Geita |
| 67 | Adinan Hussein Mbezi | Alitoweka tarehe 16 Septemba 2023 huko mkoani Geita. Hajapatikana hadi leo. | Geita |
| 68 | Lengaripo Lebahati Lukumay | Alitoweka tarehe 7 Mei 2021 huko mkoani Mwanza. Hajapatikana hadi sasa. | Mwanza |
| 69 | Akidu Twaha Salim | Alitoweka tarehe 6 Oktoba 2023 mkoani Dar es Salaam. Hajapatikana hadi sasa. | Dar es Salaam |
| 70 | Enock John Chambala | Alitoweka tarehe 6 Julai 2024 huko mkoani Tanga. Hajapatikana hadi sasa. | Tanga |
| 71 | Dioniz Kipanya | Alitoweka tarehe 26 Julai 2024 huko mkoani Katavi. Hajapatikana hadi sasa. | Katavi |
| 72 | Nusra Omari | Alitoweka tarehe 7 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam. Alipatikana akiwa amefariki. | Dar es Salaam |
| 73 | Theresphora Mwakalinga | Alitoweka tarehe 17 Julai 2024 huko mkoani Dodoma. Alipatikana akiwa amefariki. | Dodoma |
| 74 | Donald Kalist Mboya | Alitoweka tarehe 29 Juni 2024 huko mkoani Kagera. Hajapatikana hadi leo. | Kagera |
| 75 | Ilham Makoye | Alitoweka tarehe 2 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam. Alipatikana baadae. | Dar es Salaam |
| 76 | Barack Majigeh | Alitoweka tarehe 5 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam. Hajapatikana hadi leo. | Dar es Salaam |
| 77 | Joshua | Alitoweka tarehe 5 Julai 2024 huko mkoani Iringa. Hajapatikana hadi leo. | Iringa |
| 78 | Yusra Musa | Alitoweka tarehe 9 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam. Alipatikana akiwa amefariki. | Dar es Salaam |
| 79 | Angel Albert Kamugisha | Alitoweka tarehe 15 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam na baadae kupatikana. | Dar es Salaam |
| 80 | Brighton Amos Emmanuel | Alitoweka tarehe 16 Julai 2024 mkoani Dar es Salaam na kuja kupatikana baadae. | Dar es Salaam |
81 | Azory Gwanda | Alitoweka tarehe 17 Novemba 2017 Kibiti mkoani Pwani na hajapatikana hadi leo | Pwani |
82 | Ben Saanane | Alitoweka tarehe 15 Novemba 2016 Dar es Salaam na hajapatikana hadi leo | Dar es Salaam |
83 | Simon Kanguye | Alitoweka tarehe 20 Julai 2017 Kigoma na hajapatikana mpaka leo. | Kigoma |