TLS, yatoa orodha ya watu waliopotea na kutekwa na tamko juu ya ongezeko la vitendo vya utekaji na upoteaji wa watu nchini

Hadi nimeogopa,

Wamemsahau Shadrack wa Songwe aliyelipiwa faini ya 5m baadae mchongero alipotembelea mkoani naye akapotea.
Yupo kwenye orodha ametajwa.

Aliyesahaulika ni Leopold Lwajabe, aliyekuwa Boss Wizara ya Fedha, ambaye alitekwa na Kisha maiti yake inasemekana kuwa iliokotwa msituni huko Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
 
kuna orodha nimekutana nayo ya watu waliotekwa ,kuteswa au kupotea tandu 2016 - 2024 , je hii imetolewa kweli na TLS ?
Yes, ni from TLS mkuu
sijaiona kwenye website yao
Huwa wanatuma katika Email za mawakili kwanza, kisha kwenye social medias then Web


Cc: John Wickzer Mulholland
je ni kweli katika kipindi cha 2016-2020 ni watu watatu tu ?
Inawezekana isiwe watatu, lakini naamini wametaja matukio ambayo wanauhakika na ushaidi nayo tu, na si yale dhaania​
 
Haya mambo siyo ya kushabikia ipo siku yatatukuta tulioko humu
Ila kwenye orodha sijamuona
  1. MO
  2. Dr Ulimboka
  3. Kabendera kama sijakosea Kibamba
 
Nineangali hiyo list na kulinganisha vipindi viwili vya zama hizi. Kuna zama Moja inalist ndefu zaidi ya ile zama ingine.

Je huu ni mtego mwingine kwa zama hizi, "umeteka, umeumiza na kupoteza zaidi" ya zama zile, watasikika watu wakisema.

Suluhisho ni Moja.

Toa ultimatum kwa RPC wote, Makamishna wote na IGP ikifika 30th Aug 2024 wajulikane walipo wakiwa hai au mfu.

Toa ultimatum kwa vyombo vya uchunguzi ikiwemo TISS askari wote waliotajwa humo wachunguzwe kama wanauhusiano na vyombo vingine vya nje, ama makundi ya ugaidi n.k inawezekana wao ni recruiting agency ya watu wengine kuletwa mafarakano nchini au ni wahalifu TU ndani ya jeshi. lGP na DIS waongoze zoezi hilo.

Matokeo mkuu wa zama aweke hadharani kufunga jalada.

Tusisubiri ngonjera" zama zetu ni zaidi ya zama zile"
 
List ni ndefu vibaya mno
Utadhani hatuna polisi na viongozi vile.
 
Kupita ilo jedwali unaweza kuona mikoa hatari zaidi Tz .
 
Pole sana Kwa haya maswahibu.

Kilichonisikitisha zaidi ni haya mambo wanayofanyiwa Watoto wadogo aisee daa 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C-e6oeBK3R0/?igsh=MTJkMGplYnllNXd6cg==
 
Allah kareem


Yeyote aliehusika kwa watu hawa, ajue kabisa hana mkataba na Mwenyezi Mungu wa kuishi milele, kullu nafsi dhaa iqatul maut, kila nafsi itaonja mauti, na kwa Allah atakua na lakujibu mtu huyu/watu hao.
 
Sikujua kama hali ni mbaya kiasi hiki lakini kwa mwenendo huo ni dhahiri sio salama tena hapa mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…