TLS, yatoa orodha ya watu waliopotea na kutekwa na tamko juu ya ongezeko la vitendo vya utekaji na upoteaji wa watu nchini

Ndugu zangu hii inatisha sana. Takwimu ni muhimu siku zote.
Tumeishi bila kujua Ukubwa watatizo. Kumbe ni tatizo kubwa sana.

Ile ya kusikia mmoja mmoja kachukuliwa kama mbayuwayu.

Ktk Orodha iliyotolewa na TLS hapo jana idadi kubwa ya waathirika inaonekana Kanda ya Ziwa yaani Shinyanga, Geita, Mwanza na Kigoma.

Pia idadi imeonekana Dar Es Salama na Arusha ikifuatiwa na Mbeya na ama Iringa.

Takribani watu 80 wameathirika na mkasa huu. Inasikitisha na inasononesha sana.

Kwa mujibu wa Orodha iliyotaja siku na tarehe ya matukio ya utekaju au ukamataji/ upoteaji inaonesha idadi kubwa ni kuanzia mwaka 2021 na idadi ndogo sana kuanzia mwaka 2020 kushuka chini yaani 2016.

Hii inatafakarisha sana.

Mwenyezi Mungu amuinue mtu mwenye haki atamalaki juu ya Taifa hili liweze kupona.
 
Sikujua kama hali ni mbaya kiasi hiki lakini kwa mwenendo huo ni dhahiri sio salama tena hapa mahali.
List bado ndefu,hapo sijaona jina la yule jamaa aliyetekwa mitaa ya mikocheni...mfanyabiashara
Kuna wengine ni mtu na mke wake walitekwa nao muda sana
Sahv style ya kutekana imepamba moto, maana utakuta wengine wanatekwa wakati siyo wanaharakati wa kisiasa,hapo nao wana sababu zao za kutekwa

Ova
 
Swali ambalo linanitatiza ni kwa nini vyombo vya habari kote nchini vimechagua kukaa kimya kuhusu suala hili. Je, ina maana hawatambui umuhimu wa Watanzania wote kulifahamu? Wanaogopa kuliibua? Au kuna ushawishi kutoka kwa watawala unaowazuia kuzungumzia suala hili? Nieleweke vizuri, sihitimishi kwamba kimya hichi ni ushahidi wa kuhusika kwa serikali / watawala moja kwa moja, la hasha. Hata hivyo, inawezekana kwamba kuna hofu ya kuzua taharuki katika jamii yetu.

Hata hivyo, ningependekeza kwamba badala ya kuendelea kukaa kimya, serikali ingetoa kauli rasmi kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kushughulikia suala hili. Kauli hiyo ingewatuliza wananchi na kupunguza taharuki inayoongezeka, hasa kwa kuwa tayari orodha ya wahanga na wahusika imetolewa. Kwa sasa, kimya cha vyombo vya habari na serikali kinazidisha wasiwasi. Swali ni, Watanzania tunatakiwa kuelewa nini kutokana na hali hii?​
 
Umehoji mambo muhimu sana
 
Deep Down from my Heart this is the Best Comment i have never seen From You Mr Mudawote.

By saying that, i can asure you the Nation is healing soon or later..

Thank you very Much.

Umeona mbali sana.
 
Kwa kweli nimefarijika sana kuona kwamba TLS wameanza kuliangazia suala hili, wito wangu huo wameufanyia kazi kikamilifu kabisa. Yaani we acha tu, TLS hii!
Tukipata vyombo viwili vitatu vinavyomonitor maswala kama haya tutaifikisha Mbali Nchi yetu.
 
Issues ya loliondo imeumiza watu wengi Sana, kumbuka mpaka mbunge alipigwa vyuma , akanusurika kifo , chura kiziwi ni mauaji kabisa kwenye maslahi yake binafsi
 
Sometimes, silence means admission of fact.
 
Huu ujinga upo kwa sababu hakuna cha kuwafanya. Hawashtakiwi.
 
Mtego huo nani anateka watu ,tusiingizwe chaka kusema Polisi tu kumbe ata wapinzani wanaweza kutekana Ili kuifua serikali
soma vzr hilo jedwar , utaona wanachukuliww na polisi wanaojulikana kabisa , wapinzan wanamteka mtu kutoka kwa polisi?
 
JPM alisukumiziwa lawama moja kwa moja sababu ya matamko yake ya wazi wazi.

Ni tofauti na bi mdashi ambaye hana matamko kama yale ya mwendazake
 
asante Mwabukusi. AIBU KWAKO SUNGUSIA, KIBARAKA WA SERIKALI ULAANIWE. ULIKAA KIMYA MUDA WOTE
 
Sikujua kama hali ni mbaya kiasi hiki lakini kwa mwenendo huo ni dhahiri sio salama tena hapa mahali.
Hali ni mbaya sana, hali Kama hii ilikuwepo nchini Zaire (Congo DRC) enzi za Utawala wa Dikteta Mobutu Seseseko. Watu wengi waliokuwa wanakosoa Utawala wake walitekwa, kuuawa au kupotezwa kabisa na hawajawahi kupatikana hadi leo. Baadhi ya Watu wakosoaji waliobahatika Mapema kupewa taarifa za kutekwa kwao waliitoroka nchi hiyo ili kunusuru uhai wao.
Kumkosoa Rais Mobutu Seseseko ilikuwa ni kujikatia tiketi ya kifo. Naona hali kama hiyo Sasa ipo nchini Tanzania.
 
Hivi hakuna uwezekano,kila mwanafamilia akafungiwa GPS,ndani ya mwili wake,hebu wataalam tusaidieni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…