TLS Yatoa Tamko Kuhusu Maandamano ya Wananchi wa Ngorongoro, Yataka Haki Zao Ziheshimiwe

TLS Yatoa Tamko Kuhusu Maandamano ya Wananchi wa Ngorongoro, Yataka Haki Zao Ziheshimiwe

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetoa wito kwa Serikali kufuatia maandamano yaliyofanywa na mamia ya wananchi wa Ngorongoro tarehe 18 Agosti, 2024, wakidai kuheshimiwa kwa haki zao za kimsingi. Maandamano haya yalionyesha hisia kali kutoka kwa wananchi wanaopinga kuondolewa kwenye ardhi yao bila ridhaa, pamoja na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii kama shule, afya, na maji.

Katika video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, wananchi hao wameeleza masikitiko yao juu ya mazingira magumu wanayoishi baada ya kuondolewa kwenye maeneo yao ya asili. Taarifa ya TLS imesema kuwa, kwa mujibu wa Tamko la Umoja wa Mataifa la mwaka 2007 kuhusu Haki za Watu wa Asili, ibara ya 10, watu wa asili hawatakiwi kuondolewa kwa nguvu kutoka kwenye ardhi yao bila idhini yao ya hiari. Aidha, TLS imekumbusha kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 24 (1), inampa kila mtu haki ya kumiliki na kuhifadhi mali yake, haki ambayo ni ya kimsingi na isiyopaswa kukiukwa bila kufuata taratibu za kisheria.

TLS imetoa wito kwa Serikali kuchukua hatua za haraka kurejesha huduma za kijamii kwa wananchi wa Ngorongoro, ikiwa ni pamoja na kurejesha vituo vya kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura. Hii ni kuhakikisha kuwa wananchi hawa wanatumia haki yao ya kikatiba katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Novemba 2024, pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Kwa kutambua uzito wa suala hili, Baraza la Uongozi la TLS limeamua kuunda kamati maalum ya kuchunguza na kufuatilia kwa karibu mgogoro wa Ngorongoro. Kamati hiyo, ambayo inajumuisha wanasheria mashuhuri kama Dr. Rugemeleza Nshala, Tike Mwambipile, Bumi Mwaisaka, Laetitia Petro Ntagazwa, na Paul Kisabo, inatarajiwa kuchukua hatua kadhaa muhimu.

Soma Pia:
Kamati hii itaangazia kwanza kufanya mashauriano na taasisi mbalimbali pamoja na kutembelea maeneo yenye migogoro ili kufahamu uhalisia wa hali hiyo. Pia, itafanya mapitio ya sera, sheria, na mazoea yanayohusiana na umiliki wa ardhi kwa wazawa na kuhakikisha haki za msingi za raia zinazingatiwa kwa mujibu wa katiba, sera, na sheria za nchi.

Mbali na hayo, kamati itaandaa kongamano la kitaifa kuangazia namna bora ya kusimamia maendeleo huku ikilinda haki za wazawa katika ardhi zao za asili. Pia, itachunguza mashauri na hatua zilizochukuliwa kisheria ili kubaini kama kweli kuna watu waliokubali kuondoka kwa hiyari na wale waliokataa kuondoka kutoka kwenye ardhi yao ya asili.

Baraza la Uongozi la TLS limewataka wanachama wake, wananchi, na wadau mbalimbali kushirikiana na kamati hii maalum ili kufanikisha jukumu lake la kuishauri Serikali na kulinda haki za wananchi. Kamati inatarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya siku 30.

Taarifa hii imehitimishwa na Rais wa TLS, Boniface A.K. Mwabukusi, akisisitiza kuwa, TLS itaendelea kusimama kidete kuhakikisha kuwa haki za wananchi wa Ngorongoro na maeneo mengine nchini zinalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.​

IMG_6062.jpeg

IMG_6063.jpeg

IMG_6064.jpeg

20 Agosti, 2024​

TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU WITO WA WANANCHI WA NGORONGORO NA MAENEO MENGINE KUTAKA KUHESHIMIWA KWA HAKI ZAO

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepata taarifakupitia mitandao ya kijamii kwa njia ya video iliyosambaakwenye mitandao hiyo ikionyesha maandamano yaliyofanywamnamo tarehe 18 mwezi Agosti, 2024 na mamia ya Wananchi wa Ngorongoro wakidai kuheshimiwa kwa haki zao. Katika maandamano yao miongoni mwa mambo mengine, Wananchi hao wamesikika wakilalamikia kuondolewa kwenye maeneoyao kinyume na utaratibu bila wao kuridhia pamoja nakuondolewa kwa huduma zote za kijamii kama vile shule, huduma za afya pamoja na maji. Kutokuwepo kwa hudumahizi muhimu kumepelekea Wananchi hao kuendelea kuishikatika mazingira magumu.

Tamko la Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Watu wa Asili la Mwaka 2007 limeeleza wazi katika ibara ya 10 kwamba watuwa asili hawataondolewa kwa nguvu kutoka kwenye ardhi au maeneo yao, uhamisho wowote wa watu wa asili hauwezikufanyika bila idhini yao huru

Kwa mujibu wa ibara ya 24 (1) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kila mtu anayo hakiya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo. Haki ya kumiliki mali ni moja ya haki ya msingi ya binadamu. Ibara 24 (2) imeeleza wazi kwamba mtu yoyotehatonyang’anywa mali yake isipokuwa kwa kuzingatiataratibu za kisheria ikiwepo ulipwaji wa fidia stahiki.

TLS inatoa rai kwa Serikali kuonyesha nia yake ya dhati kwakurudisha huduma zote za kijamii kwa Wanachi waNgorongoro kwa kuwa ni haki yao. Pia, vituo vyakujiandikisha kwa ajili ya kupigia kura ambavyo Wanachi waNgorongoro wanalalamika

kwamba havipo katika maeneoyao virudishwe ili wapate kuitumia haki yao ya kikatiba yakujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwa ajili ya uchaguziwa Serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwezi Novembamwaka 2024 pamoja na Uchaguzi mkuu utakaofanyikamwaka 2025.

Baraza la Uongozi la TLS limeona jambo hili la Ngorongoro na maeneo mengine linahitaji ufuatiliaji wa kina zaidi na kwasababu hiyo, Baraza limeamua kuunda kamati maalumitakayofuatilia jambo hili kwa ukaribu ikiwa ni pamoja nakuwasiliana na Idara, Wizara na vyombo vyote vinavohusikana suala la Ngorongoro ili kujua ukweli zaidi na kuhakikishamisingi ya sheria za nchi yetu inafuatwa.

Kamati iliyoundwa inajumuisha wajumbe wafuatao:​
  1. 1Dr. Rugemeleza Nshala
  2. Tike Mwambipile
  3. Bumi Mwaisaka
  4. Laetitia Petro Ntagazwa na
  5. Paul Kisabo.
Miongoni mwa mambo mengine kamati itafanya mambo yafuatayo:​
  1. Kufanya mashauriano na taasisi mbalimbali pamoja nakutembelea baadhi ya maeneo yenye migogoro ili kujuauhalisia wa migogoro husika.​
  2. Kufanya Mapitio ya Sera ,Sheria na Mazoea pamoja nakuzichambua kuhusiana na umiliki wa Ardhi kwa Wazawa pamoja na shughuli za uwekezaji na Uhifadhi na kubaini uzingativu wa Haki za Msingi za Raia katikamaeneo husika kwa kuzingatia Katiba, Sera na Sheria za Nchi.​
  3. Kuandaa kongamano (Symposium) la Kitaifa kuhusianana namna bora ya kufanya maendeleo kwa kuzingatia nakulinda haki za Wazawa katika Ardhi zao za Asili pamoja na haki zao za Kijamii, Kiuchumi naKiutamaduni katika maeneo yanayofikiwa na shughuli za uwekezaji.​
  4. Kubaini mashauri au hatua zote ambazo zimechukuliwana walalamikaji pamoja na walalamikiwa kisheria nakiutaratibu katika kuhakikisha uzingativu wa sheria nakubaini majina ya watu ambao kweli wameridhiakuondoka kwa hiyari kwenye maeneo yao na ambaohawakuridhia kuondoka kwa hiyari kwa sababu ya wao kuamua kubaki katika eneo lao la asili Ngorongoro.​
  5. Kubaini na kulishauri Baraza la Uongozi la Chama Cha Mawakili wa Tanganyika juu ya hatua zakuchua ilikupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu swala la migogoroya Ardhi inayosababishwa na mipango ya uwekezaji au uhifadhi.​
Kamati inatarajiwa kumaliza kazi tajwa ndani ya muda wakipindi cha siku 30.

TLS inawaomba Wanachama, Wananchi pamoja na wadaumbalimbali wa Sheria kutoa ushirikiano kwa Kamati maalumiliyoundwa ili TLS kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungucha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act Cap. 307) iweze kutimiza wajibu wake wa kuishauri Serikalina Kulinda haki za Wananchi kwa lengo la kupata suluhishola kudumu.​

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Boniface A.K Mwabukusi
Rais​
 
Kanjunjumele apewe shavu aache njaa na kelele.
 
NGORONGORO WORLD HERITAGE, NI LAZIMA IHIFADHIWE, NO MATTER WHAT, HAKUNA NAMNA, "NGORONGORO MUST LIVES FOREVER WITH NO DISTURBANCE" / KIMSINGI NGORONGORO NI NCHI YA WANYAMA PORI, BINADAMU ALIJIPELEKA TU KWA NJAA ZAKE "
 
Kanjunjumele apewe shavu aache njaa na kelele.
Kenyetta alisema watanzania ni maiti hawaezi kufufuka. Mtu mzimahuwezi kuandika haya,ni MAITI tu anaweza andika haya
 

Attachments

  • KENYATTA.mp4
    3 MB
Kenyetta alisema watanzania ni maiti hawaezi kufufuka. Mtu mzimahuwezi kuandika haya,ni MAITI tu anaweza andika haya
inawezekana Mwabu ana interest zake za kisiasa, ila ni ukweli kwamba kwa sasa Taifa linahitaji strong TLS kuliko wakati mwingine, na moja ya nguzo ya kuifanya TLS iwe imara ni kuwa na Rais mwenye uthubutu kama Mwabu, labda Michewen atuambie ameona nini hadi kusema hayo 🤷🏽‍♂️​
 
inawezekana Mwabu ana interest zake za kisiasa, ila ni ukweli kwamba kwa sasa Taifa linahitaji strong TLS kuliko wakati mwingine, na moja ya nguzo ya kuifanya TLS iwe imara ni kuwa na Rais mwenye uthubutu kama Mwabu, labda Michewen atuambie ameona nini hadi kusema hayo 🤷🏽‍♂️​
Nyerere aliipenda taifa lake, lakini si kuwa Nyerere hakuhitaji kula, kuvaa, kusomesha watoto etc etc, essential human need..amenities of life! Mwabu is not an exception, LAKINI KUNA CAUSE HALALI ANAIPIGANIA KWA MANUFAA YA WOTE
 
Kwan walikuwepo kwanzia lini?🤔
Nature inatueleza waliishi binadamu na wanyama, katika Proportionality fulani, kitendo cha binadamu kuzidi au kuwa wengi mno, hapa ndipo tatizo linapoanzia!, kwa sababu binadamu temepewa akili ya utambuzi ni lazima tuone tu nafanyaje, ukizingatia Tanzania ina ardhi isiyo hifadhi kubwa ya kutosha basi baadhi wa masai wapunguzwe huko!
# BILA MIHEMKO HII NI POINT YA MSINGI KABISA!
 
Hawa nao kila siku wanatoa tamko halafu wanapotea hakuna wanachofanya!! Ukisikia unafki ndo huu!!!
 
Back
Top Bottom