Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli na msimu wa mvua za masika zitakazoishia Aprili 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 31, 2024, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a alisema mvua za chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi kutokana na mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa. Mvua hizi zinatarajiwa kuanza kwa kusuasua katika maeneo ya Ziwa Victoria na kuenea hadi maeneo mengine mwezi Oktoba.
Pia, Soma: Hizi Bilioni 24.5 walizopokea Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa (TMA) zitatumikaje kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi?
Katika msimu wa Vuli (Oktoba hadi Desemba 2024), mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani katika mikoa ya Kaskazini na maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
Aidha, kwa msimu wa masika (Novemba hadi Mei), mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, na baadhi ya maeneo ya Lindi, huku mikoa ya Singida, Dodoma, na maeneo ya Kanda ya Magharibi kama Tabora na Kigoma yakitarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Dk. Chang’a alisisitiza umuhimu wa kufuatilia utabiri wa kila siku na kila mwezi ili kupata taarifa za kina kuhusu mwenendo wa mvua na vipindi vya mvua kubwa.