TMA: Kupatwa kwa Jua hakutakuwa na athari zozote kwa Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema leo Aprili 8, 2024 dunia inatarajia kushuhudia tukio la Kupatwa kwa Jua Kikamilifu ambapo Mwezi utazuia kabisa Mwanga wa Jua, hata hivyo tukio hilo halitakuwa na athari zozote kwa upande wa Tanzania

TMA imesema nchi zitakazoshuhudia zaidi tukio hilo ni za Bara la Amerika Kaskazini kupitia Mexico, Marekani na Canada. Kwa upande wa Tanzania hali hiyo haitaonekana kwasababu iko eneo la mbali kutoka njia ya Kupatwa kwa Jua Kikamilifu.

Unakumbuka nini katika Matukio ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi?

Screenshot_2024-04-08-14-10-21-642_com.google.android.apps.docs-edit.jpg
 
Duh! TMA inahusika vipi na kupatwa kwa jua, jua, mwezi na nyota viko anga za juu, mbona kama wanavuka mipaka? Wao si wana deal na hewa iliyopo humu humu ndani ya anga la tanzania? Labda kungekuwepo na mamlaka ya anga za juu ingefaa watuambie haya, angalau hata mamlaka ya usafiri wa nga kidogo wanafaa kutuambia habari za anga zikoje huko juu.
 
Kama anahusika na taifa stars kufuzu afcon,anahusika na simba na yanga kwenda robo fainali kwann na hili lisimhusu?
hili la kupatwa kwa jua liko anga za juu, ni tofauti na stars, simba na yanga
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema leo Aprili 8, 2024 dunia inatarajia kushuhudia tukio la Kupatwa kwa Jua Kikamilifu ambapo Mwezi utazuia kabisa Mwanga wa Jua, hata hivyo tukio hilo halitakuwa na athari zozote kwa upande wa Tanzania

TMA imesema nchi zitakazoshuhudia zaidi tukio hilo ni za Bara la Amerika Kaskazini kupitia Mexico, Marekani na Canada. Kwa upande wa Tanzania hali hiyo haitaonekana kwasababu iko eneo la mbali kutoka njia ya Kupatwa kwa Jua Kikamilifu.

Unakumbuka nini katika Matukio ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi?

View attachment 2957812
Nakumbuka sir henry ,Quarter man bwana na umbopa walipomuonyesha miujiza kigagula king solomon mine!
 
Kuna mwaka hili tukio litatokea tanzania, wataalam wameshapiga hesabu za mambo ya mienendo ya mwezi na jua angani
 
Duh! TMA inahusika vipi na kupatwa kwa jua, jua, mwezi na nyota viko anga za juu, mbona kama wanavuka mipaka? Wao si wana deal na hewa iliyopo humu humu ndani ya anga la tanzania? Labda kungekuwepo na mamlaka ya anga za juu ingefaa watuambie haya, angalau hata mamlaka ya usafiri wa nga kidogo wanafaa kutuambia habari za anga zikoje huko juu.
Unaelewa maana ya Mamlaka ya Hali ya Hewa?
 
Kwanza kabisa nipende kumshkuru mh raisi kwa kazi nzuri anayoifanya hasa katika kufanikisha zoezi Hili la kupatwa kwa jua🤣, hakika mama yenu anaupiga mwingi 🤣😂😂
 
Asante Mama Samia umewezesha dunia kushuhudia tukio hili kubwa duniani
 
Back
Top Bottom