Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Soma hapa Wanasayansi wa Hali ya Hewa Waonya kwamba EL-Nino Itakayotokea Mwaka Huu Itakuwa Mbaya kuliko Zote Zilizowahi Tokea hapa Duniani | JamiiForums Tanzania https://share.google/fjcF74ttlqhewYueMMamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Niño kuanzia Septemba na kuendelea hadi Oktoba, Novemba na Desemba 2026, huku athari zake zikitarajiwa kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2027.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 18, 2027 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Ladislaus Chang’a amesema uwepo wa El Niño yenye nguvu unaweza kusababisha vipindi vya mvua kubwa pamoja na kuanza mapema kwa mvua za msimu katika baadhi ya maeneo.
Chang’a amezitaka Idara na Taasisi mbalimbali Nchini, ikiwemo Mamlaka za Bandari, reli, usafiri wa anga pamoja na Sekta ya Afya, kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
“Tunatoa maangalizo mawili la kwanza ni kutokana na uwepo wa El Nino yenye nguvu kubwa kuelekea Mwezi Oktoba, Novemba na Disemba na mwanzoni mwa 2027 vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuanza Septemba pamoja na mvua za vuli, pia kuwepo kwa El Nino kunaweza kusababisha kuanza mapema kwa mvua za msimu,”.
September imepita hakuna kitu zaidi ya mawingu tu asubuhi mchana jua kali sanauwepo wa El Nino yenye nguvu kubwa kuelekea Mwezi Oktoba, Novemba na Disemba na mwanzoni mwa 2027 vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuanza Septemba pamoja na mvua za vuli, pia kuwepo kwa El Nino
Mshukuruni Mungu hata kwa hapa, bado kuna watu wanakesha wanaombea nchi, so mvua kuwepo or kutokuwepo ni jambo la kupiga magoti kwa Mungu kuomba toba aturehemu.Kumbe walisema kunzia septemba?
Sasa tuko octoba 3 dalili bado hazijajitokeza!
Hatukatai uwepo wa hizo mvua ila zinaweza kuwa si mvua kubwa kama wanavyo tabiri
Naam ashukuriwe sana mwenyezi Mungu na watiwe nguvu wote wanao omba kwa Mungu hali iwe kawaida.Mshukuruni Mungu hata kwa hapa, bado kuna watu wanakesha wanaombea nchi, so mvua kuwepo or kutokuwepo ni jambo la kupiga magoti kwa Mungu kuomba toba aturehemu.
Lakin haimaamishi TMA ni waongo. Ukiona haijaja , upige goti kwa Mungu na kusema Asante
Kumbe jua kali, joto, na ukame ndiyo mvua nyingi? Au TMA walisoma utabiri baada ya kupata cha mafinga?Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Niño kuanzia Septemba na kuendelea hadi Oktoba, Novemba na Desemba 2026, huku athari zake zikitarajiwa kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2027.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 18, 2027 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Ladislaus Chang’a amesema uwepo wa El Niño yenye nguvu unaweza kusababisha vipindi vya mvua kubwa pamoja na kuanza mapema kwa mvua za msimu katika baadhi ya maeneo.
Chang’a amezitaka Idara na Taasisi mbalimbali Nchini, ikiwemo Mamlaka za Bandari, reli, usafiri wa anga pamoja na Sekta ya Afya, kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
“Tunatoa maangalizo mawili la kwanza ni kutokana na uwepo wa El Nino yenye nguvu kubwa kuelekea Mwezi Oktoba, Novemba na Disemba na mwanzoni mwa 2027 vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuanza Septemba pamoja na mvua za vuli, pia kuwepo kwa El Nino kunaweza kusababisha kuanza mapema kwa mvua za msimu,”.
Sio mvua tena, TMA wamesema itakuwa ni El Nino ya joto kali na ukame, hivyo bilioni 700+ zilizotengwa zitatumika kukabiliana na athari za joto kali 🤔Ahsante kwa taarifa, uzuri kwa sasa TMA wana vifaa vya kisasa sana, taarifa zao ni za uhakika