TMA yatabiri mvua za wastani lakini yatoa angalizo mvua kubwa ya vipindi vifupi katika msimu wa Machi-Mei 2023

TMA yatabiri mvua za wastani lakini yatoa angalizo mvua kubwa ya vipindi vifupi katika msimu wa Machi-Mei 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Ladislaus Chang’a ametangaza mwelekeo wa msimu wa mvua za masika zinazoanza Machi mpaka Mei, 2023 ambazo zinatarajiwa kuwa za wastani huku baadhi ya mikoa kuwa wastani na juu ya wastani.

TMA.jpg
MWENENDO WA MVUA ZA MSIMU (NOVEMBA, 2022 HADI APRILI, 2023) NA MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA (MACHI – MEI), 2023

Mwenendo wa mvua za Msimu (Novemba, 2022 hadi Aprili, 2023)

Mvua za Msimu zilizoanza mwezi Novemba, 2022 katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka (mikoa ya Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro) zilinyesha kwa kiwango cha wastani katika kipindi cha Novemba, 2022 hadi Januari, 2023. Mvua hizi zilitawaliwa na vipindi virefu vya ukavu hususan mwezi Novemba, 2022 kwa maeneo ya pwani ya kusini, na kusini mwa mkoa wa Morogoro. Katika kipindi kilichosalia cha msimu (Februari, Machi na Aprili) mvua zinatarajiwa kuendelea kama ilivyotabiriwa mwezi Oktoba, 2022.

Mwelekeo wa mvua za Masika (Machi hadi Mei), 2023
Msimu wa mvua za Masika ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), pwani ya kaskazini (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Kutokana na mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa katika kipindi cha msimu (kama inavyoelezwa katika kipengele cha 2 cha taarifa hii), kwa ujumla mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga pamoja kisiwa cha Pemba katika msimu wa mvua za Masika, 2023. Hata hivyo, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia), kaskazini mwa mkoa wa Morogoro na kisiwa cha Unguja. Ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Mei, 2023 katika maeneo hayo. Maelezo ya kina juu ya mwelekeo wa mvua hizo za msimu ni kama ifuatavyo:

Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, na Mara) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo):
Mvua za Masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi, 2023 na zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Mei, 2023.


Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mkoa wa Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba):
Mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia), kaskazini mwa mkoa wa Morogoro na kisiwa cha Unguja.

Aidha, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa kunyesha katika maeneo ya mkoa wa Tanga pamoja kisiwa cha Pemba. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi, 2023 na kuisha Juni, 2023.

Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani na zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi, 2023. Mvua hizo zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2023.
 
TMA inatakiwa itoe ushauri kwa wakulima wapande mazao gani na watumie mbegu gani
TMA waachwe wasimamie masuala ya hali ya hewa,au kwani hiyo mamlaka inaripoti kwa nani maana ikibidi hivyo basi iwe chini ya wizara ya kilimo wanakohusika na mambo hayo.
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa taarifa ya Utabiri wa Mwelekeo wa Mvua za Msimu wa Masika zinazotarajiwa kuanza mwezi Machi hadi Mei 2023 unaonesha kuwa baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam itapata mvua kubwa kuanzi wiki ya pili ya mwezi huo.

newslite1648721032441.jpeg


Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA, DK Ladslaus Chang’a amesema kutokana na hali ya miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam ni vyema Mamlaka husika zikajiandaa ili kueopusha athari zitakazojitokeza ikiwemo mafuriko.

 
Foleni itakuwa ya hatari kwenye barabara zinazojengwa za kilwa na Nyerere itakuwa balaa ...
Acha tusubiri tuone itakuaje
 
Ukisikiliza vizuri hakuna la maana kaongea! Hawa ndiyo wataalamu wetu. Wastani ni nini, kidogo ni nini?



You are right, hawa ni takataka na hakuna vyombo vya kupima hayo ywaliyoyasema /vilivyowapa taarifa hizo, wamekaa ofisini and they cooked that stupid information..... bure kabisa , takataka
 
Upuuzi mtupu wala hakuna kitakachotokea maana ni data za kuoka ie cooked data!
 
Back
Top Bottom