Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza utabiri wa mvua kubwa katika mikoa 11, itakayoanza leo, Novemba 30, hadi Desemba 1, 2024.
Maeneo yatakayoni mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, na Rukwa), ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi (Lindi na Mtwara), Kanda ya Kati (Dodoma na Singida), Kanda ya Kusini (Ruvuma), pamoja na Mkoa wa Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA leo, Novemba 29, 2024, hali mbaya ya hewa inatarajiwa kuendelea kwa siku tano kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 3, 2024.
Mamlaka imewataka wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa zaidi kuhusu hali ya hewa.
Source: Mwananchi