TMA yatoa angalizo la mvua kubwa inayoweza kusababisha makazi kuzungukwa na maji

TMA yatoa angalizo la mvua kubwa inayoweza kusababisha makazi kuzungukwa na maji

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

tma.jpg

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa bahari ya Hindi (Mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Kati mwa nchi (Mikoa ya Singida na Dodoma), Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi) na Nyanda za Juu Kusini magharibi (Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa na Njombe).

UWEZEKANO WA KUTOKEA: MDOGO

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: KUBWA

Athari zinazoweza kujitokeza: Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.

Zingatia na jiandae.
 
Haya huku Mbeya wanaoishi ISYESYE,ITUHA,na ITEZI waanze kuhama sasa😎
 
Watu wanaoishi maeneo yanaweza kukumbwa na mafuriko wanatakiwa kupewa elimu ya namna ya kuepuka janga la mafuriko ikowezekana wahamishwe kabisa.
 
Back
Top Bottom