Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,346
Kiukweli wadau ningependa kusikia hoja zenu hapa!
Nb: Matusi na dharau sio ustaarabu!
Free ideas naanza kukuuliza mimi:
Ikiwa Hakuna Mungu, na wale manabii walikuwa ni magreat thinker tu waliodeclare utume ili kupitipisha theory zao, embu niambie ni kwanini kunautabiri wa kweli ktk vitabu vitakatifu?
Nb: Matusi na dharau sio ustaarabu!
Ok nakujibu kwa ufupi,
Katika historia,inaonesha watu wa ukanda wa mashariki ya kati na maeneo kama misri,Jordan,kwenda mpaka Ugiriki,Walikuwa watu wa kwanza kuvumbua maandishi na mambo ya kalenda na hata hesabu.
walikuwa na utaalam wa kusoma nyota na unajimu hata vipindi na majira mbalimbali pia.Waliweza pia kutunza kumbukumbu kwa maandishi ambayo pia wao ndo waliyavumbua.Hii ilikuw miaka mingi iliyopita.
kwa hiyo matukio na mambo mbalimbali yaliyofanyika katika jamii zao yaliweza kuandikwa na kuwekwa kama kumbukumbu.masimulizi kutoka kizazi hadi kizazi pia.
Kutokana na kuwepo kwa kumbukumbu sahihi ya maisha ya mababu zao,taifa la izrael linakuwa na kurithi misingi ama maonyo ama mafundisho ya kizazi kilichopita.
Izrael ilikaa utumwani misri miaka kama mia 400,lakini kwa sababu ya kutunzavkumbukumbu,walijua kwamba sio asili ya pale misri.Na katika harakati za kujikomboa na UTUMWA,ndipo watu mbalimbali maarufu na wanamapinduz kama akina MUSA,JOSHUA,ARON na wengine wanawakumbusha waizrael kwamba asili yao sio pale na inabidi warudi nchi ya mababu zao.Katika hili zinatungwa falsafa nyingi kama ilivo kwa marevolutionarist wengine waliopita.,Kwa nchi YA AHADI,NCHI YA MABABU ZETU,NCHI YA ARDHI TAKATIFU,INAYOTIRIRIKA ASALI NA MAZIWA,TAIFA TEULE n.k.Yaan ni kama akina kinjekitile kwamba motto ni ,,,MAJI,,,Ama BACK TO AFRICA MOVEMENT.(hapa watanielewa wale walio na free ideas tu,wengine mtaona nakufuru).
Baada ya muda mrefu musa anafanikiwa kuwarudisha wana wa Izrael katika ardhi ya mababu zao japo yeye hakufika kuyokana na umauti ulomfika wakiwa njiani.,Baada ya wao kufika mambo yanaendelea kamabkawaida lakini kumbuka taifa hili limejengwa kayikabmisingi ya Imani ya kuambiwa nabkusimuliwa.
Idea ya mungu MMOJA inajitokeza pia baada ya kuonekana watu wanatengeneza vinyago nakuviabudu.Viongozi wakaona tuseme kuna mungu mmojabambaye haonekani ili kusiwe na ULINGANIFU KATIKA MIUNGU,MAANA KULIKUWA NA MIUNGU WA SHABA,DHAHABU,ALMASI n.k,na kila mmoja alikuwa anaonekana muhimu hasa kutokana na jinsi alivotengenezwa.So ile kusema kuna mungu. mmoja ilikuwa ni Defensive mechanism ili kuwafanya watu waogope kwa kuwa mungu haonekani.
Katika kuendeleza Imani yao,walizaliwa watu mbalimbali waliokuta jamii ya Izrael inaendelea na utamadun wa kuabudu na kiimani,na kutokama na maandiko ya kiimani na kihistoria na mfumo wa maisha kwa ujumla,mtoto yoyote alitakiwa kujua mafundisho haya na ndicho kilikuwa kinafundishwa mashulen na katika masinagogi.,
Ahadi ya kuzaliwa mkomboz ni inabaki kuwa fumbo tangu enzi za nabii Elias ,Mkomboz anatabiliw akutokna na mateso ya waizrael misri na utumwani kwa ujumla.Laini mkombozi YESU(kama n kwel),anakuja kuzaliwa tayar wakiwa kwao na anazaliwa katika hali wasiyoitarajia.Yesu akasema katoka kwa mungu wakamuua.
kwa hiyo hapa point ni kwamba mitume na manabii walitoka Mashatiki yabkati kutokana na kuw ana kumbukumbu za ahadi walizojiwekewa wenyewe kujifariji kutokana na maisha magumu. na ile kutawaliwa,so kila mtu akawa anakuja na falsafa yake.
Kutokana na kumbukumbu pia Anazaliwa Mohamed ambaye nae anadai ametumwa na Allah kuja kueneza habar njema.Hii pia ni kutokana na historia kwamba wao kama wao(waarabu) ambao kumbukumb zao zinaonesha nivkizazi cha Ismael ama labda ESAU nao wanajikakamua baada ya miaka 600 ya kufa yesu.Mwaka 632,AD,anazaliwa Mohamed kisha baadae anasema Ametokewa na Allah wakati akiwa bonden(pango) na mkewe.Basi anaandika misingi ya maisha nabkupata wafuasi ambao ndo waislam wa leo.Lakini hii yote ni kutaka kuonesha kwamba na sisi tunaweza,ama kwa nn wao tu ama ccje?,ama kutimiza historia amavkujipa moyo maana zamani hakukuwa na kingine cha muhimu sana tofauti na Mambo ya imani na kusoma sheria za vitabu vya mababu kama musa,Ibrahim n.k.Na waliweza kufanikiwa kutokana na ujinga wa watu wa enzi hizo waliokubali ya kuambiwa"",Eti mungu kanitokea nikiwa pangoni kanambia mimi ndo ameniteua niwe mtume wake"",afu pangoni aliwa yeye na hadija mkewe,ushahidi uko wapi??.miaka hii pia kuna wanao sema hayo lakini wanapuuzwa kwa sabau si zama z aujinga na upumbavu hiz.Watu watataka evidences zilizoshiba.Ulishawahi kujiuliza kwa nn mungu hawashukii watu tena siku hizi?.ulishawahi kujiuliz akwa nn Manabii na mitume hawaji tena?.tafakar
Turudi katika historia,Marekani imetawaliwa karibu miaka 400,sawa na Israel,lakini unajua kwa nn marekan hawakuwa na wakombozi ama mitume ama manabii?.sababu ni hizi..
Marekani haikuwa ,ama haikutunza kumbukumbu za mababu zao vizazi vingi vilivopita kama izrael.Marekani ilikuwa tangu mwanzo mchanganyiko wa makabila na mataifa mbalimbali,kwa hiyo hakukuwa na itambaduni wa jumla katika jammii,mtakumbuka red Indians,Marekani hakukuvumbuliwa maandishi mapema kama ilivokuwa Misri,Izrael na ukanda ule kwenda mpaka Greece.Hakukuw ana cctim yabkuamini amavkuabudu kma mashariki ya kati.Hizo ni baadhi tu ya sababu japo zipo kibao.
hakika nakwambia Ikiwa akina SHAKHA ZULU,V.I LENIN,MAHTIMA GHANDI,ISACC NEWTON,ALBERT STEIN na wengine kma hao,wangesema wametoka kwa mungu ama yale wayafanyayo ni kaz ya MUNGU leo tungekuwa na newtonism,steinism n.k.na iwapo wapigania uhuru wengine sehem zingine wangeandikwa kwenye vitabu enzi hizo bas hata akina musa tusingewasikia sana kama leo hii .naona niishie hapo kwa sasa kama kuna swali uliza ..
Free ideas naanza kukuuliza mimi:
Ikiwa Hakuna Mungu, na wale manabii walikuwa ni magreat thinker tu waliodeclare utume ili kupitipisha theory zao, embu niambie ni kwanini kunautabiri wa kweli ktk vitabu vitakatifu?