To You..

klorokwini

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
8,647
Reaction score
5,145
aaah! mods naomba mic niwakilishe.

oh! baby!

nimekaa na kutulia, mengi nimefikiria
Mawazo yamenijia, tangu tulipoanzia
shairi nakutungia , nielewe my dia
mwenzio ninaumia, please say wewe pia

Kila nikikuangalia, kweli umekamilika
nguvu zinaniishia, nikuite malaika?
moyoni ninaumia, mwenzio nasononeka
Penzi lako nalilia, usije wakakuteka

Natamani kuwa nawe, sekunde kila dakika
Liwalo acha na liwe, moyoni nimekuweka
Mola acha asifiwe, alokuumba ukaumbika
Daima mimi na wewe, wazi wazi natamka

Napenda sauti yako, ukitaja jina langu
Hufichi hisia zako, ukiwa pembeni yangu
Kukusaliti ni mwiko, umetosha kiu yangu
Milele mimi ni wako, kwavile wewe ni wangu.

Nasifu zako tabia, Wazazi nawapa sifa
Mtoto umetulia, akili na maarifa
"Honey! nimekupikia", unanipa taarifa
Darling nimekuzimia, nakupa zote nyadhifa.

Usiku ukiingia, mapema wajitayarisha
Visa wanisimulia, vyengine vya kuchekesha
Uchokozi waishia, na kuanzisha tamasha
Nami nalimalizia, na koja nimekuvisha.

Macho ukiniangalia , taabani sijiwezi
mwendo u kitembea, laniuwa lako pozi
Nyumbani nakungojea, fanya hima laazizi
Zawadi mekuletea , za kukupa usingizi.

Nina mengi ya kusema, lakini muda hautoshi
Nakuombea uzima, Uzidi wako ucheshi
Unithamini daima, kwa harusi na mazishi
Ewe changu chema, Unukiae marashi.

Ni malenga wenu klorokwini a.k.a ileile "bukta la jeshi"
 
¿¿¿¿¿¿.........???????
Kumbe Kloro una kipaji hivi??

Nimekusikia mpenzi tabasamu langu pokea
Shukurani nakupatia mazuri yangu kuyatambua
Kwa zako nzuri tabia moyo wangu nakupatia
Leo hata na kesho mimi ni wako tambua!

Utashi wako adimu mwenyewe wajijua
Kila nikiwa nawe maisha nafurahia
Wenye wivu wachukia mioyo yao yaumia
Leo hata na kesho mimi ni wako tambua!

Wambea wanaongea furaha kutuondolea..
Kila wakijaribu uvivu twawatolea...
Kamwe hatushawishiki mabaya kuyasikia
Leo hata na kesho mimi ni wako tambua!
 
Natamani kuwa nawe, sekunde kila dakika
Liwalo acha na liwe, moyoni nimekuweka
Mola acha asifiwe, alokuumba ukaumbika
Daima mimi na wewe, wazi wazi natamka


shukrani dawa ya Malaria:biggrin1::biggrin1:
 
Kudadekii hapo kwenye bluu ankal sijui ulikuwa unafanya nini
 
Aah Kamanda hupati mtu hapa hahaha!
 
Dearest huyu ni mtu wa nne kumpokea kwenye ile club yetu sasa ratiba itakuwaje ?
 
Hahahahhaha dearest hapa najibu mapigo tu bwana....Kloro is not mine to keep!!!Mliopo mnanitosha!!
Afadhali ingekuwa vizuri hata hao wengine wawili wakachukuliwa na mafuriko ya mvua hizi za sasa lol!
 
Jamani dearest kumbe hupendi nifurahi ehhhh???!
Jamani Liz furaha yako kutupanga mafungu ? utachakaa mapema na watakimbia wote ila mimi niliosema hata at 50 bado nitakupenda.
 

Lemme say wow, mistari imetulia
I might sell my cow, zawadi kukupatia
I love u more now, wapi ulisomea?
U wanna make me bow, mikono kukuinulia.

Nilificha lako jina, to play guess game
Hukuogopa fitina, never mind the blame
Kwa mapana tena sana, U mentioned your name
Sina hata la kunena, Your picture is in my brain frame.
 
Reactions: mja
Natamani kuwa nawe, sekunde kila dakika
Liwalo acha na liwe, moyoni nimekuweka
Mola acha asifiwe, alokuumba ukaumbika
Daima mimi na wewe, wazi wazi natamka


shukrani dawa ya Malaria:biggrin1::biggrin1:

heheeh I hope umepona sasa
 
Reactions: mja
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…