To You..

PHP:



Shairi limetulia, kwa vina kupangilia
mtoto wamsifia, moyoni washangilia
malaika wamdhania, na penzi walilia
mapenzi yana hadaa, ndugu yangu klorokwini

mapenzi yana ghiliba, ndugu yangu tahadhari
yasije geuka mwiba, na mengi yenye shari
wengine wakaja iba, waile yako sukari
mapenzi yana hadaa, ndugu yangu klorokwini

Nyadhifa zote wampa, eti umedhamiria
siku akija kutupa, wapi utakimbilia
je akigeuka papa, ni vipi utatwambia
mapenzi yana hadaa, ndugu yangu klorokwini

Tabia zabadilika, kama upepo masika
leo yu malaika,namba wani ameshika
vipi akija kuchoka, na mapenzi kuyazika
mapenzi yana hadaa, ndugu yangu klorokwini

Hapa natamatia, namini umesikia
ni vyema kuzingatia,yaweza kusaidia
mola akupe na nia, usipatwe na kadhia
mapenzi yana hadaa, ndugu yangu klorokwini



Hahaha.....namimi naweza nikawa malenga
 
Yaaani Kloro kaanzisha sredi???
Tena li-Songi la Awilo Longomba??
Kudadadadadadadada deki zake, kweli sasa amepona.

hehehe Lokassa ya mbongo! Hizi anga za Klorokwini a.k.a director wa Titanic wewe unatafta nini? wewe acha nikuwekee wimbo unaokuhusu hapa chini. Uskilize kwa makini halaf ulipe hela yangu haraka.

 
Last edited by a moderator:
Breaking News: Klorokwin In Love lol

Hakika amesikia, kiliocho kakipata
Anatikisa mkia, moyoni kakupakata
Raha anaisikia, mawingu umeyakata
Sema baba usikike, usijekufa kwa kihoro............................
heheh na huyu ndio mjukuu mtiifu. Kumbe na mistari ipo? aiseee!
 
klorokwini unatishia mzee hii mistari ni balaa, du ngoja nami niandike nitarudi....


Mkuu umekubalika, katika hii hii fani
Mistari imetukuka, tukuite namba wani?
Mwenyewe nimetishika, Naogopa kusaini
Kwangu usiwe na shaka, najipa matumaini

Mapenzi ni usanii, babu aliniusia
Jifanye kuwa mtii, mapenzi kukumbatia
Lakini yakikuudhii, haraka mbele timua
Mapenzi ni ulaghai, Lugha tamu kutumia

Nikisema sili sinywi, hivi nitaishi vipi?
Ila kama hadanganywi, atakuthamini vipi?
Atakuona nyang'anywi, takataka za makapi
Lugha mapenzi haifinywi, Hata nepi yaitwa chupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…