Toa jibu la chemsha bongo hii

20PROFF

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
8,186
Reaction score
7,184
Naomba mnisaidie sababu ya hii hesabu hapa chini . . . . Nilikua na Tsh.50/-

MATUMIZI SALIO
20/- 30/-
15/- 15/-
9/- 6/-
6/- 0/-
….… ………
50/- 51/-

Hili tofauti/ongezeko la Tsh 1 linatokea wapi?
Mkuu wa chuo, pita hapa,
 
Last edited by a moderator:

Hesabu yako hii haijakaa vizuri, ulikuwa una shilingi 50... lakini kwa hapo chini umepanga sehemu ya matumizi pamoja na salio, na jinsi ulivyojumlisha umejumlisha sivyo, sehemu ya matumizi upo sawa...

kwa sababu kupata jumla ya salio ni sawa na matumizi yako yote ndio unapata salio lenyewe ndio maana imekaa sawa... Hesabu yako ipo sawa kabisa, lakini ninaposema haijakaa vizuri ni hapo ulipokosea kujumlisha upande wa kulia, ndio maana imetokea hiyo tofauti...
 

Hebu itazame, katika matumizi na kinacho bakia, utaelewa nilichokuwa nafanya
 
Hebu itazame, katika matumizi na kinacho bakia, utaelewa nilichokuwa nafanya

Haukubakia na kitu angalia hiyo zero, kwenye hiyo series yako... ulikuwa na sh 50 ukatumia 20 ukabakia na 30 hapo upo sawa, katika hiyo 30 ukatumia 15 ukabakia na 15 hapo upo sawa, katika hiyo 15 ukatumia 9, ukabakia na 6 ukaitumia hiyo 6 ukabaki na 0 hapo bado upo sawa...

Sasa basi unapokosea unapochukua jumla ya yale masalio ambapo unapata 51 unatoa na yale matumizi ambayo kimsingi yanakuja 50 na hiyo ndio ipo sawa ndio maana unapata tofauti ya 1, unapojumlisha yale masalio ndio error inapotokea...
 
Jumla ya ulichotumia= salio lako la mwanzo, lakini jumla ya yale masalio uliyokuwa unabaki nayo haiwezi kuwa sawa na salio lako la mwanzo... Hebu tuliweke tofauti tuone, hiyo hiyo sh 50...

Matumizi Masalio
30/- 20/-
15/- 5/-
5/- 0/-
... ......
50/- 25/-

Umeona ninachomaanisha!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…