Toa Maoni yako Juu ya Katiba Mpya kupitia Tovuti ya TUME

Toa Maoni yako Juu ya Katiba Mpya kupitia Tovuti ya TUME

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408
WATANZANIA TUTOE MAONI YETU KUHUSU KATIBA MPYA KATIKA SEHEMU HIZI:
1. Unaweza kutembelea tovuti ya tume ya katiba na ukatoa maoni yako. Tembelea Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utoe maoni yako.
2. Tuma sms ukianza na kutaja jina lako,umri na mahali unapoishi. Kisha toa maoni yako
a. 0715 08 15 08
b. 0767 08 15 08
c. 0787 08 15 08
d. 0774 08 15 08
Hizo hapo ni njia rahisi za kutoa maoni yako juu ya katiba mpya na hazina gharama yoyote kubwa jamani.
Kumbuka mustakabali na uhai wa taifa hili upo mikononi mwako.

Kwa ufupi kuna mambo mengi ya kuzungumza mf.
1. Nini maoni yako juu ya madaraka ya rais? yapunguzwe au yaongezwe au yabaki vilevile?
2. Nini maoni yako juu ya aina ya muungano tulionao? Muungano ubaki hivi hivi au tuwe na serikali 3 au hizi mbili?
3. Nini maoni yako juu ya serikali za majimbo? ziwepo au zisiwepo?
4. Nini maoni yako juu ya wabunge kuwa mawaziri? je ni sawa au sio sawa?
Na mengine mengi......tafadhali changia maoni yako. Uhai wa taifa hili upo mikononi mwetu.
 
Fursa hii ni adimu ......


- kizazi kijacho kitayapiga viboko makaburi yetu kila asubuhi ndo waende kutafuta riziki. Katiba ndio riziki na maisha ya binadamu duniani ...... tutumie fursa hii inayoweza kupatika mara moja tu kwa karne moja
 
Back
Top Bottom