Kwanza waambieni hao waendesha kongamano wawaache watu wawe huru kuongea chochote cha mambo ya elimu, Halafu wataalamu wa mitaala baadae watachambua humo chuya ni zipi na mchele ni upi, wasianze kurestrict watu maana siyo kila mtu humo ni mtaalamu wa mitaala.
Baada ya hayo nina mchango ufuatao:
A: Pamoja na mitaala mizuri, bado tunahitaji vitu vya kuifanya mitaala ifanye kazi kwa ufanisi huko mashuleni(Yaani means to backup school curriculums for the maximum efficiency), Hii ina maana namna ya kuwainvolve wadau wote wa elimu waplay role yao vizuri, Hapa tunahitaji kumuinvolve mzazi na MALEZI
B: Pili tunahitaji namna ngani nzuri ya kudeliver hiyo mitaala mashuleni, kwa hiyo hapa kuna umuhimu wa kuinvolve ICT, Walimu, Watu wenue uelewa wa masomo kuvolunteer kufundisha in their spare time, hapa lazima Wizara itunge kanuni za kuvuna human resource yote iliyoko nchini inayotaka kusaidia
Kwa hiyo kiufupi nima maoni yafuatayo:
1)TUNAHITAJI SERA YA TAIFA YA MALEZI.
Mheshimiwa, elimu kwa mtoto huanza mara tu atuapo duniani baada ya kuzaliwa na mamaye, kwa hali ilivyo sasa sehemu kubwa ya ulezi ameachiwa mzazi hususan mama, kama mama ana mbinu bora za ulezi zenye kuchochea udadisi na ufahamu wa mtoto basi mtoto hunufaika, lakini kama mzazi hajui mbinu za kumfanya mtoto wake awe na vitu hivyo basi mtoto huishia kuwa wa kawaidakawaida. TUNATAKIWA TUWE NA MUONGOZO WA ULEZI ili kuwapa mbinu wazazi jinsi ya kuwaongoza watoto wao wenye umri let say miaka 1-5, 6-10, 11-15, 16-17, kila kundi lijue vitu kadhaa wa kadhaa, kama vile, utu, bidii, nidhamu, heshima, udadisi, kazi kadhaa za mikono, kauli nzuri, etc hii itasaidia sana kujenga taifa lenye watu walio na msingi mzuri tena common kwa taifa zima. ELIMU YA MSINGI PEKE YAKE HAITOSHI, INAHITAJIKA SERA YA TAIFA YA MALEZI., Ili mitaala huko mashuleni iweze kufanikiwa, lazima tuweke input zetu kwenye malezi
2) KUHUSU MASOMO YA SAYANSI TUMIA WATU WANAOJUA JAPO SIYO WAALIMU.
Kuna watu nchi hii wanajua sana masomo ya Sayansi lakini kutokana na wao kuchagua kazi nyingine wao siyo waalimu, hata hivyo nikitazama upungufu wa waalimu wa Sayansi, ni muda muafaka kwa Wizara kuona inawatumiaje watu hawa waliotapakaa nchi nzima kuokoa jahazi hili wakati serikali ikiendelea kutengeneza walimu wake huko mavyuoni. Mtu aliyepata A au B ya hesabu, Physics, Chemistry au Biology kidato cha sita enzi hizo huyo ni hazina ya Taifa, Tukubali kuwapa Part Time Job hawa watu Watusaidie mpaka pale mambo yatakapikaa sawa.
3) SHIRIKISHA MIFUMO YA IT
Kama Wizara ikitengeneza Web System, Halafu Walimu wazuri wakarekodi materials yakawekwa katika system, na Agizo likatolewa kila shule iwe na Computer angalau Ishirini, Sasa hivi kwa speed ya Internet na umeme uliotapakaa nchi nzima Vijana wetu wanaweza kunufaika na mifumo hii. Hapa niseme tu, kuwa Hawa Walimu wataalamu siyo lazima wawe Watanzania, anaweza akawa yeyote duniani ilimradi lafudhi yake inaweza kueleweka vyema na wanafunzi wetu.
5) SHIRIKISHA WAALIMU WA VYUO.
Huko mavyuoni kuna watu kutokana na Nature ya Kazi yao kuhitaji GPA kubwa, basi hawa ni watu ambao mara nyingi walikuwa vizuri sana kimasomo toka elimu za awali, kwa nini wizara isifinance Postgraduate Diploma ya Education kwa kila Academician mwenye Interest ili hawa watu in their spare time waende wakawafundishe na wadogo zao huko?, NI LAZIMA TUMAXIMIZE THE UTILIZATION OF OUR RESOURCES. Kuna kipindi vyuo huwa vinafungwa miezi minne, Je kwa Academicians hususan Ma T.As na Assistant Lectureres kwa muda huo hawawezi kuwa wamesaidia kukata topic kadhaa kwa wadogo zao huko vijijini kwenye uhaba wa Walimu?.
6) Mheshimiwa, KUNA BAADHI YA VITABU VINATAKIWA VIWE VYA ZIADA.
vitabu kama vile vya Taasisi ya Elimu vya hesabu vilivyokuwa vikitumika takribani miaka 20 iliyopita vya form 1 mpaka form 4 vilikuwa ni vitabu vizuri mno, Ongea na wadau mheshimiwa uone ni namna gani hivyo vitabu vinarudi katika mitaala, na pia kuna vitabu Classic kama vile vya Abbot, Lambert, Roger Muncaster, Bannet, mama hivi ni lazima viwepo katika Library ya Kila Shule.
7) VIJANA WANAOKWENDA/WANAOMALIZA JKT WANAWEZA KUTUSAIDIA
Kwa sasa tunajenga Labs, na pia tuna upungufu wa Walimu, lakini kule JKT wanapoenda vijana wetu kupigishwa kwata kuna baadhi ya vijana ni very bright, wana passes nzuri sana, na wakiwa trained wanaweza kutusaidia sana katika shule za kata huko interior huko, Kwa nini basi hawa badala ya kwenda kupigishwa kwata National Service yao ikawa ni kwenda kusimamia Labs, au Kufundisha ikibidi?,Ili kuwamotivate hawa vijana unaweza kuwapunguzia/kuwaondolea ada ya masomo yao pindi wakianza universities.
Time is running against us, we must run while they are walking, natambua ugumu lakini Tukisema tusubiri mpaka tuwe na Walimu wale Professional wachukue nafasi, tutasubiri kwa miaka 10 ambayo kimsingi tutaipoteza.