Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Maisha ya mahusiano ni matamu sana, kama utapata mtu sahihi. Na utamu wake, muwe mnasikilizana; na sio kumfanya mtoto wa mwenzio kuwa mzazi wako, kwa kumbebesha majukumu ambayo hata wazazi wako waliyashindwa.
Kutoka toka 'out' kunanogesha sana uhusiano; hasa ile 'out' ya kulala huko muendako. Hotel, lodge n.k hizi zote zimejengwa kwa ajili yetu; na ukizitumia vizuri zinaboresha mahusiano mliyo nayo.
Si lazima, mpaka muwe mmefunga ndoa ndio mtoane 'out'; Itategemea na aina ya uhusiano mlio nao. kwa sababu, mahusiano ya kiutu uzima yapo ya aina nyingi; yapo ya kupeana kampani tu, yapo ya kuja kuoana baadaye, na pia yapo ya mume na mke.
Kwa hiyo jitahidini sana, kutoana 'out' hasa za mbali, iwe za kuvuka mikoa, wilaya, nchi n.k; kufanya hivyo kunanogesha uhusiano wenu; pia unakuwa umeipumzisha akili vizuri, na pia kuongeza uwezo mkubwa wa kufikiri namna ya kujiongezea kipato.
Utakuta katika mahusiano mnakuwa na mahasira hasira ya ajabu ajabu, yasiyokuwa na tija, muda wote mnanuniana, mara mwingine analalamika apelekewi moto, mara mwingine apikiwi n.k; hii inatokana na kutokutoana 'out'.
Toaneni 'out', kwa uhai wa mahusiano yenu.