Toba ndani ya ndege....

Malcolm X5

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
1,639
Reaction score
2,752
Msamaha wa kweli unahitaji Neema ya Mungu. Sikiliza hii,

Kuna jamaa mmoja na Mkewe walikuwa wanasafiri kuelekea Italia kwa safari ya kibiashara kwa ndege. Wakiwa angani likatoka tangazo kwamba injini zote za ndege hazifanyi kazi sawasawa hivyo muda si mrefu ile ndege itadondoka, hivyo kuwasihi abiria kuomba sana pamoja na kutubu kwa ajili ya kujiandaa na kifo ambacho kwa vyovyote kilikuwa hakiepukiki.

Yule jamaa akamgusa mkewe na kumwambia, honey naomba unisamehe maana yule mdogo wako tunayeishi nae amekuwa mpenzi wangu kwa muda mrefu sana, na tayari ameshatoa mimba nyingi tu, na tulikuwa na mpango wa kukuua. Hivyo naomba unisamehe.

Mkewe akamjibu, hakuna tatizo dear nimeshakusamehe, kwa kuwa ni kipindi cha kutubu basi ngoja na mimi nikiri mbele yako uovu niliokutendea. John na Esther sio watoto wako, mtoto wako ni Victoria, pia siku ile ulivyoporwa fedha na majambazi, mimi ndiye niliyeandaa huo mpango ili nilipie ada ya Chuo ya mpenzi wangu Juma, hata sasa nilikuwa na mpango wa kukuua ili nirithi mali. Jamaa akamwambia mkewe nimekusamehe.

Wakati huo huo, tangazo likatoka kwamba, tunashukuru abiria kwa maombi yenu, Mungu ametusikia na sasa tunauhakika wa kufika salama safari yetu, Asanteni sana. Pamoja na tangazo hilo ambalo lingewafanya wafurahi, lakini abiria wote walikuwa kimya. Ndipo yule jamaa alipopaza sauti rubani! rubani! lazima uiteketeze hii ndege ukishindwa tutaiteketeza wenyewe.

Abiria wote wakajibu kwa pamoja, ndioooooooooooo!!
 
hahahahahaaaa,kama nawaona hivi abiria walivosawijika nyuso zao!
 
Mchezo nini?,kwanza hapo ndoa zote hakuna tena
 
Hii inanikumbusha kuna baba mmoja alikua anaumwa, tena alikua na nafasi kubwa tu kanisani. Hali ilikua mbaya sana kiasi kwamba ndugu na jamaa walikata tamaa ya kupona kwake. Ikafika kipindi baadhi ya wazee ikabidi waende kwa mgonjwa na kumwambia kuna kitu chochote ambacho ungependa tukifahamu? Alitaja watoto kama sita hivi ambao amewazaa nje ya ndoa na mkewe alikua hajui, akataja kwa majina na mama zao. Wakati huo watoto waliokua wanajulikana kwa mkewe wa ndoa ni watatu tu.

Bahati nzuri yule jamaa akapona ule ugonjwa, hali ilikua mbaya sana!
 
@samalitan hakukaliki tena ndani,wameongezeka wa3 eheheh
 
Dah kwel nimeani hakuna anae ogopa kufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…