Sina tafsiri rasmi, zaidi ya jinsi ninavyoyaelewa.
Usharika ni neno nimelisikia zaidi kwa upande wa kidini, hasa mgawanyiko wa maeneo ya kanisa. Mfano, Kinondoni, kuna makanisa kadhaa labda Hananasif, Shamba. Sasa haya makanisa yatajulikana kama usharika. Ikitokea kuna mkusanyiko, watatofautishwa kwa kuwaita usharika wa Hananasif, usharika wa Kinondoni Shamba.
Ushirika ni umoja, muungano we aina fulani ili kutekeleza jambo/ lengo pamoja.