Tofauti hii kubwa kati ya Watoto wadogo wa Kiswahili / Kitanzania na wale wa Kizungu ( Ulaya / Marekani ) inatokana na nini hasa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ukipata bahati ya Kukutana na Watoto wadogo wa Kitanzania ( Kiswahili ) maongezi yao mengi watakayokukaribisha nayo hayatokuwa yanacheza mbali na haya:

" Uncle GENTAMYCINE jana Wenzako tumekula Ubwabwa huo "
" Uncle GENTAMYCINE leo asubuhi Baba Kajamba huyo "
" Uncle GENTAMYCINE mpaka muda huu hatujala Kitu Baba amefilisika "
" Uncle GENTAMYCINE siku ya Kula Nyama Baba huwa anawahi kweli kurudi Nyumbani "
" Uncle GENTAMYCINE Mama leo kapigwa hadi kanyimwa Chakula "
" Uncle GENTAMYCINE naomba Hela nikanunue Ice Cream na Golori "
" Uncle GENTAMYCINE umeshawahi kucheza Kibaba baba na Kimama mama? "


Ukiipata bahati hiyo hiyo na ukakutana na Watoto wadogo wa Kizungu ( Ulaya / Kimarekani ) maongezi yao mengi watakayokukaribisha nayo hayatokuwa yanacheza mbali na haya:

" Uncle GENTAMYCINE so far how many Books have you read? "
" Uncle GENTAMYCINE what is the strongest planet amongst all? "
" Uncle GENTAMYCINE do you like President Trump and his leadership style? "
" Uncle GENTAMYCINE what kind of Tourism attractions can be found in Tanzania? "
" Uncle GENTAMYCINE next time when you come to visit us get ready to give us Nyerere's History "
" Uncle GENTAMYCINE how many types of Fish can be found on Lake Victoria? "
" Uncle GENTAMYCINE why do you love CCM instead of CHADEMA or CUF or ACT? "


Naomba kujua hii tofauti kubwa kama inavyoonekana hapo juu imetokana / inatokana na nini?

Nawasilisha.
 
Na Pia ukikutana na mazungumzo ya Vijana wa Kitanzania utasikia:

(Tababata siku kuna viwanja vikali watoto wakali balaa. Mi pale BL na The Great nishawatafuna sita, hadi ndogo oya oya tu).
 
Mimi niseme tu hayo yaliotajwa hapo hasa yanatokea kwa vizazi ambavyo wazazi wao ni hali duni kiuchumi.
Hadi unakuta anapolala baba kikisikika kitu, watoto wanasikia upande wao walio lala.

Best thing tupambane na hii kitu inaitwa poverty.

Na ndio kwanza wananchi wanazid kudorola, sikukuu sasa naona watoto ni kudorola tuu, biashara watu wanauza vitu kwa faida ndogo kabisa ilimradi apate ulaji na yeye maana wateja ni wachache,
Nilienda kununua kuku wa x-mass juzi kati aisee kuku ambae kipindi kingine huanzia 15 had 20 yan waliniuzia elfu tisa tisa.
Na wanunua kuku walikua wachache balaa sio kama sikukuu zingine
 
Sikuhizi watoto wetu wamebadirika kidogo kwa sababu wanaanza chekechea mapema
Hiyo ilikuwa zamani Toto linamiaka 8 haijui shule unafikiri ataongea nini
 
Na Pia ukikutana na mazungumzo ya Vijana wa Kitanzania utasikia:

(Tababata siku kuna viwanja vikali watoto wakali balaa. Mi pale BL na The Great nishawatafuna sita, hadi ndogo oya oya tu).
Hahaa humo humo
 
Nimecheka sana " lakini huu ndio ukweli wenyewe " hayo uliyo yaeleza kuhusu watoto wa tz yamenitokea leo " ....

Mida ya jioni ya leo nilikuwa manzese kuna mtu nilikuwa na shida nae nikamfuata huko " ... basi bwana palikuwa na watoto kadhaa wanacheza pembeni yao walikuwa wamekaa mama zao " ... basi kati ya wale watoto akatokea mmoja akamuuliza mwenzake " X yuko wapi " .. Yule aliyeulizwa akajibu amekwenda KUDANGA " ... Aisee nilipigwa na butwaa ghafla " mama mmoja kati ya wale wazazi wawale watoto akaanza kumkaripia yule mtoto " lakini tayari alikuwa amesha waiibisha " kwamba hawana malezi bora yenye nidhamu kwa watoto wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…