Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Baking powder na baking soda zote vinatumika kwa kazi moja ya kuumushia au kuchachua chakula kama mkate, cake, biskuti na baadhi ya vyakula lakini vina tofautiana kikemikali. Baking soda kwa jina lingine ni BICARBONATE OF SODA .
Asili yake ni alkalini. Kama uliwahi kufanya majaribio shule kipindi hicho ukichanganya baking soda na asidi kama siki( vinegar) ilikuwa inatoa mapovu. Hii ni kwa sababu alkalini ikikutana na asidi hutoa gesi aina ya kaboni dioksaidi inayosababisha hayo mapovu na ndio maana inaumua chakula chako.
Mapishi mengi yenye kutumia baking soda yanakuwa na mojawapo ya asidi kama vile siki, limao au ndimu, maziwa mala au mtindi. Fuata vipimo sahihi vya baking soda, ukikosea na kuzidisha kama ilikuwa ni cake basi haitaumuka na itakuwa na ladha ya uchungu.
Baking powder ni mchanganyiko wa baking soda ambayo imechanganywa na asidi kavu na unga wa mahindi ili isipate kuumuka hadi pale itakapopata joto ndio itaanza kuumuka. Baking powder hutumika kwenye mapishi mengi na haina ulazima wa kutumia viungo vyenye asidi ili ipate kuumuka, muhimu ipate maji au joto la jiko ndo inapoanza kufanya kazi.
Tumia baking powder ilokuwa imehifadhiwa vizuri na ambayo haijapata baridi ili kupata matokeo mazuri. Tunashauriwa kuhifadhi baking soda na baking powder sehemu kavu, isokuwa na jua ili isipate kuharibika. Fuata masharti ya kwenye kila pishi ikihitajika baking soda utumie kama ilivyo na ikihitajika baking powder pia uitumie kama ilivyo, na iwapo kama vitahitajika vyote viwili kwenye pishi moja tumia kufuatana na vipimo vilotolewa usizidishe.
Ikiwa imekaa mda hujatumia na unatakuwa kujua kama bado inafaa chukua baking soda kidogo weka kwenye bakuli tia siki kidogo kama itatua mapovu ujue bado inafaa. Kwa baking powder tia kwenye bakuli na maji kidogo ikijaa inamaanisha bado nzima.
Picha namba 1, 2 na 3 ni aina za baking powder rahisi kupatikana hapa nchini. Picha namba 4 na 5 ni baking soda. Hupatikana kwenye maduka yote ya mitaani, maduka wanayouza vyakula na hata supermarkets