Tofauti kati ya Difu yenye reduction na Diffu ya kawaida ni ipi?

Tofauti kati ya Difu yenye reduction na Diffu ya kawaida ni ipi?

king henry

Member
Joined
Sep 2, 2018
Posts
10
Reaction score
7
Tunajua ili gari ifanye kazi vema na ihimili mwendo ni razima kuwe na difu madhubuti. Naomba msaada kujua tofauti ya difu ya kawaida na difu yenye reduction
 
Siongelei gari za kisasa zinazovuta mbele Naongelea gari ambayo ili itembee lazima kuwe na nguvu inayosafirishwa kutoka kwenye gearbox kwenda kwenye difu na kusambazwa katika wheel
Kuna gari hazina diff
 
Siongelei gari za kisasa zinazovuta mbele Naongelea gari ambayo ili itembee lazima kuwe na nguvu inayosafirishwa kutoka kwenye gearbox kwenda kwenye difu na kusambazwa katika wheel
Hata gari zinazovuta mbele zina diff
 
Kuna tofauti nyingi, ila kubwa ni kwamba axle yenye reduction inasaidia gari kuwa na ground clearance kubwa kuliko ambayo haina reduction. Kama ulishapita kwenye barabara mbovu, mara nyingi gari za juu kama kina Land Cruiser zinapokwama, ukichungulia chini unakuta diff ndio imenasa kwenye udongo, hasa pale unapokusea "ukaweka kati" gema au tuta. Gari yenye reduction axle ule mtungi wa diff unaweza kuwa mdogo au unaweka kuwa juu, sio usawa mmoja na axle.
 
Mimi ndiyo najua leo kwamba kuna reduction diff na non reduction diff.

Mimi ninazoziona ni reduction diff. tu. Yaani kunakuwepo na pinion (small gear) inayoendesha crown wheel (large gear).
 
Kwanza tungetoana matongotongo kidoogo,
diff ya kawaida ni ipi na diff ya reduction ni ipi.

Mimi binafsi ufahamu wangu upo kwenye maroli.najua kuna lori zenye lock diff na kuna zenye reduction diff.
Ila kwenye gari ndogo sijui kitu.

Sasa humu jf wajuvi ni wengi,pengine hata mimi ufahamu wangu kwenye diff za malori haupo sawa.
Wataalam waje watujuze mawili matatu.
 
Diff zote zinafanya reduction, pale gear ndogo (pinion) itakapo muendesha gear mkubwa (ring gear/crown) hapo ndipo reduction hutokea au nguvu huongezeka.
 
Back
Top Bottom