Tofauti Kati ya Kawi na Nishati

Tofauti Kati ya Kawi na Nishati

MwendaOmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2013
Posts
774
Reaction score
723
Mara nyingi mie nilikuwa najua ya kwamba maneno "Nishati" na "Kawi" yana maana moja ila Nishati ni TZ na Kawi ni Kenya (Kumaanisha Energy.)

Hivi majuzi, nilimskia mtangazaji nchini Kenya akisema, "Hamna upungufu wa nishati Katika sekta ya Kawi." Kuna mtu ambaye anaelewa maana ya sentensi hii?

Na hiki ni kitendawili kwa wa tz. Mkiskia mtu anuliza,

Nini sasa na wewe? au
Na nini sasa wewe?
Sasa nini wewe?
wewe sasa nini?

Utaelewa maana yake? Au Kiswahili hiki pia kinatumika TZ?
 
Neno KAWI ni kifupi cha kilowatt ambacho ni kipimo cha nishati (energy), kama ilivyo kilogram kuwa kipimo cha uzito.
Lakini Kenya wanatumia hili neno KAWI pia kumaanisha NISHATI.

Kwa maoni yangu huyo mtangazaji hakukosea. Kusema "Hamna upungufu wa nishati Katika sekta ya Kawi" nadhani alimaanisha kuwa katika sekta ya nishati, hakuna upungufu (wa nishati).

Kitendawili:
Katika matumizi ya lugha mitaani (slang) unaweza kulegeza kanuni. Ni kama kusema:
Whats up = What is up = Mambo aje, au Ni aje, au Nini sasa na wewe? (pengine hii inaeleweka Kenya)
 
Kawi nm [i-/zi-] (Kenya) = Energy.

Hii ni kwa mujibu wa KAMUSI ya TUKI ... sasa hiyo ya kuita "kawi ni kifupi cha kilowatt" hapo huyu jamaa Kifyatu anataka kutuingiza mjini

cc: MwendaOmo Kifyatu
 
Kawi nm [i-/zi-] (Kenya) = Energy.

Hii ni kwa mujibu wa KAMUSI ya TUKI ... sasa hiyo ya kuita "kawi ni kifupi cha kilowatt" hapo huyu jamaa Kifyatu anataka kutuingiza mjini

cc: MwendaOmo Kifyatu

Ni sawa unavyosema lakini kawi = KW au Kilowatt.

Jiulize hii kamusi ya TUKI umepataje hili neno KAWI kumaanisha ENERGY?
 
Back
Top Bottom