Mara nyingi mie nilikuwa najua ya kwamba maneno "Nishati" na "Kawi" yana maana moja ila Nishati ni TZ na Kawi ni Kenya (Kumaanisha Energy.)
Hivi majuzi, nilimskia mtangazaji nchini Kenya akisema, "Hamna upungufu wa nishati Katika sekta ya Kawi." Kuna mtu ambaye anaelewa maana ya sentensi hii?
Na hiki ni kitendawili kwa wa tz. Mkiskia mtu anuliza,
Nini sasa na wewe? au
Na nini sasa wewe?
Sasa nini wewe?
wewe sasa nini?
Utaelewa maana yake? Au Kiswahili hiki pia kinatumika TZ?