tofauti kati ya ''kodi'' na ''ushuru''

tofauti kati ya ''kodi'' na ''ushuru''

Architect E.M

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
1,222
Reaction score
1,425
wapendwa wanajamvi, ninaombeni msaada wenu wa dhati katika kutofautisha hayo maneno
 
Kodi hulipwa kwa kipindi maalum, ama kwa mwezi au hata kwa mwaka! Ushuru hulipwa kila siku!!!

Ni mtizamo tu
 
Kodi ni tozo linalotolewa baada ya kufanya biashara na kupata faida halafu asilimia fulani iliyowekwa ndio unalipa lakini Ushuru ni tozo unalotoa kabla hujapata faida, huangaliwa thamani ya kitu au mali hiyo na kulipia asilimia fulani ya gharama ya hiyo mali. Ni mtazamo na uzoefu wangu tu, nasubiri kukosolewa.
 
Jinsi ninavyoelewa tofauti:
* Ushuru ni malipo yanayodaiwa na serikali kulingana na thamani ya bidhaa zinazoingizwa nchini; utekelezaji kwa kawaida uko mkononi mwa idara ya forodha mpakani au bandarini.
Mfano: mafuta yananunuliwa nje ya nchi yanafika mpakani yakiwa na bei ya sh. 1000 kwa lita. Serikali inadai ushuru wa asilimia 30 kwa hiyo gharama ya lita tayari kwa mfanyabiashara imeshakuwa sh 1300 huko mpakani.

* Kodi ni malipo yanayodaiwa na serikali kulingana na kiwango cha mapato ya watu au makampuni, au kulingana na thamani ya biashara (VAT)
 
Kodi na ushuru ni vitu vinavyofanana, ila kodi malipo kwa serikali kutokana na vitendo vilishokwisha fanyika wakati ushuru ni malipo kwa serikali ili kupata uhalali wa kufanya vitendo fulani nchini.
 
huwa nasikia maeneo ya sokoni wanatozwa ushuru. Hata yule zakayo alikuwa mtoza ushuru. Na mmesema ushuru unahusishwa na imports. Tufafanulieni hapo
 
Back
Top Bottom