Tofauti kati ya kusikia na kusikiliza.

Tofauti kati ya kusikia na kusikiliza.

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
747
Reaction score
1,454
Wajuzi wa lugha naombeni mnipe tofauti kati ya haya maneno mawili , Kusikia na kusikiliza.
 
Mi sio mjuz sana wa lugha ila kwa uelewa wangu ni kwamba kusikia ni hali ya kusikia kila sauti inapokuwepo bila kujali kipi haswa umesikia

Kusikiliza ni hali ya kuelewa yote uliyosikia,maana unaweza kusikia usielewe bt ukatumia muda kusikiliza ukapata uelewa..

Ndio maana hata kiingezeza yamejitofautisha haya maneno
Listen
Hear
 
Jambo/kitu muhimu unakisikiliza na ni rasmi kabisa Ila kusikia ni kama dharula tu
 
Wajuzi wa lugha naombeni mnipe tofauti kati ya haya maneno mawili , Kusikia na kusikiliza.
Kusikia (hearing) ni ile hali ya ukamilifu wa masikio kupokea mawimbi ya sauti kwa sababu mtu sio kiziwi.
Kusikia huja bila jitihada yeyote kwa sababu tu mtu yupo mahali penye mawimbi fulani ya sauti.

Kusikiliza (Listening) ni taaluma ya lugha ambapo mtu hutumia kanuni mbalimbali kutega sikio ili kupata kusikia na kutafsiri mawimbi fulani ya sauti yanayofika kwenye masikio na kupata maana mahsusi.
 
unaweza kusikia usisikilize..uwezi kusikiliza bila kusikia nikiwa namaanisha kusikia ni kitendo cha sikio la nnje kukusanya sauti nyingi lakini huishia apo apo kwenye sikio la nnje..mf.ukiwa sokoni kuna sauti nyingi sana unaziskia lkn uzielewi kwa kuwa ujazitilia maanan

kusikiliza ni kitendo cha kusikia sauti kwa kutumia sikio la nnje na kuziruhusu kwenda kwenye ubongo ili kutafsiriwa..mf.ukiwa sokoni unaskia sauti nyingi ila unaweza komaa na moja hivyo kuwezesha kutafsiriwa vyema
 
Back
Top Bottom