Mr. MTUI
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 8,130
- 8,362
'Composition' ya maziwa ya wanyama inategemeana na aina ya mnyama. Mungu aliweka composition tofauti kwa kila aina ya maziwa na mnyama husika ili maziwa yaweze kumwezesha kiumbe mdogo 'aliyezaliwa' aweze kukua na kufikia ukubwa unaostahili na kwa muda unaotakiwa.
Composition nayoongelea hapa ni virutubisho kama vile protini, wanga, mafuta,vitamini na madini.
Kutokana na nilichongea hapo juu hii inamanisha kwamba maziwa yanayofaa zaidi kwa mtoto mdogo ni maziwa ya mama yake na si vinginevyo.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba maziwa ya wanyama wengine kama vile maziwa ya ng'ombe, mbuzi, kondoo au maziwa ya unga hayapaswi kupewa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kutokana na sababu mbalimbali na sbabu kubwa ikiwa ni utofauti wa virutubisho uliopo kwenye maziwa mbadala. Ingawa kiwango cha maji kilichopo kwenye maziwa ya wanyama na binadamu kinafanana kunautofauti mkubwa wa viwango vya virutubisho vingine.
WANGA NA PROTINI
Kiwango cha carbohydrate, protini na mafuta kilichopo kwenye maziwa ya wanyama kama vile tembo, ng'ombe, nyangumi, binadamu n.k kinapaswa kikidhi mahitaji ya mnyama husika, mfano; kiwango cha protini kwenye lita moja ya maziwa ya ng'ombe ni gramu 3.3 wakati kwenye kila lita maziwa ya binadamu yana gramu 0.9 za protini. Hii inamanisha kwamba kiwango cha protini kwenye maziwa ya ng'ombe ni zaidi ya mara mbili.....😵😵😵😵 ya kilichopo kwenye maziwa ya binadamu..
Hii ni kwasababu kiwango cha protini kwenye maziwa kinategemeana na muda unaotakiwa na mnyama husika kukua hadi kujitegemea...kiwango kikubwa cha protini husaidia mwili kukua haraka. Mtoto mchanga haitaji protini nyingi sana kwani ukuaji wake ni wa taratibu na badala yake huitaji mafuta 'fat' kwa wingi kwani kiwango kikubwa cha nguvu 'energy' hutumika mwanzoni katika kusaidi ukuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mifumo ya fahamu......😉😉😉
Kuna mifano mingi sana ya wanyama ambao wanakua haraka sana mfano;
PANYA-kiwango cha protini kwenye maziwa ya panya ni gramu 11 kwenye kila lita moja, na panya huchukua siku nne kuongezeka mara mbili ya ukubwa/ uzito wake wa awali ' wa kuzaiwa'
PAKA 'NYAU'-maziwa ya NYAU yana gramu 8.9 kwenye kila lita moja, kutokana na hili huchukua siku 10 kuongezeka mara mbili ya uzito, au ukubwa wa awali wa kuzaliwa.😀😀😀😀
NG'OMBE-Maziwa ya ng'ombe yana gramu 3.3 kwenye kila lita moja, kutokana na hili huchukua siku 40 kwa ng'ombe kuongezeka mara mbili ya uzito wake wa kuzaliwa.
BINADAMU-maziwa ya binadamu yana gramu 0.9 kwenye kila lita moja ya maziwa, kutokana na hili huchukua siku 180 kwa binadamu kufikia mara mbili ya uzito wa kuzaliwa.
Utofauti mwingine...
Maziwa ya wanyama yana kiwango kikubwa cha casein ambayo ni ngumu kumeng'enywa na hii pia ni moja ya sababu inayofanya maziwa haya yasifae kwa watoto wadogo.
MAFUTA
Kiwango cha mafuta kilichopo baina ya maziwa ya ng'ombe na binadamu kinafanana ingawa utofauti upo kwenye aina ya mafuta yaliyopo.
CALCIUM
Maziwa ya ng'ombe yanakiwango kikubwa cah madini ya calcium kuliko maziwa ya binadamu...hi inatokana na sababu kwamba ng'ombe wana 'skeletoni' au mifupa mikubwa kuliko binadamu hivyo madini ya calcium yanahitajika kwa wingi ili yaweze kusaidi katika ujenzi na uimarishaji wa mifupa yao. Maziwa ya binadamu yanakiwango kidogo cha madini ya calcium kutokana na maumbile yao kuwa madogo. Hii pia ni sababu inayofanya maziwa ya ng'ombe yasifae kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja.
.
MADINI YA CHUMA 'IRON'
Maziwa ya ng'ombe yanakiwango kidogo cha madini ya chuma ukilinganisha na maziwa ya binadamu. Hii pia ni sababu inayochangia kutokufaa kwa maziwa ya ng'ombe kwa watoto wadogo.
JE UNAWEZA TENGENEZA MTINDI KWA KUTUMIA MAZIWA YA MAMA?😱😱😱😱😱😱
Jibu ni ndiyo..maziwa ya mama kama yalivyomaziwa ya ng'ombe yanaweza tumika kutengenezea mtindi kwa ajili ya watoto wao kwa njia ya uchachushaji 'fermentation'...utofauti utakuwa kwenye uzito wa mtindi na muda utakao hitajika kuyachachusha hayo maziwa na kufikia ubora unaohitajika.