Tofauti kati ya Mfanyabiashara na Mfanyakazi (Mtumishi wa Umma)

Tofauti kati ya Mfanyabiashara na Mfanyakazi (Mtumishi wa Umma)

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2019
Posts
491
Reaction score
1,010
Kitu nimechogundua katika safari yangu ya maisha baada ya ku experience vyote viwili kwa muda mrefu, ni kwamba kuna tofauti kubwa ya wasomi hasa watumishi na wafanya biashara. Miongoni mwa tofauti hizo ni

1:Elimu , biashara inahitaji skills na skills una experience while ajira nyingi za bongo zinaangalia vyeti vya knowledge na knowledge una learn .hapa naomba nieleweke vizuri., Elimu pote inahitajika bali elimu itayokusaidia katika biashara ni uzoefu utakaoupata kutokana na shughuli zako za kila siku. Hivyo Elimu zetu za vyeti zinatupa uzito kufanikisha biashara kwasababu hazina mahusiano ya moja kwa moja na uhalisia wa biashara

Kwahiyo hata kama umesomea biashara ila ili uwe mfanya biashara unahitajika ufanye kwanza biashara (u experience) kwa vitendo uachane na utajili wako wa kwenye diary .Biashara ina mambo mengi tofauti na tunavyofundishwa hivyo ili uyajue lazima uwe umewahi kuifanya na sio unakuta mtu hajawahi kuuza hata Karanga afu anajikuta Bakhresa.

2: Ujasiri/ roho ngumu. Biashara inahitaji roho ngumu kupita maelezo. Mfanya biashara suala la kupata na kukosa ni kitu cha kawaida, habari za kupiga hasara, kuzulumiwa na kukata upepo ( mzigo hautoki) ni sehemu ya maisha yake. Mtu yeyote alie kwenye biashara kwa muda mrefu huwa anaujasiri usio kipimo mana anayoyapitia ni zaidi ya vita vya kijeshi. Ila wenzangu na mimi hatuna presha tuna count tarehe tu , kama kipindi hichi najua michomekeo itakuwa mingi mtaani.

3. Biashara inahitaji umakini wa hali ya juu kuliko. Najua kuna kazi nyingi zinahitaji umakini mkubwa katika kuzifanikisha ila biashara ni kiboko. Kuna msemo mzee wangu anapenda kuusema kuwa "akili zunguluka mali potea" yani kibiashara haijalishi biashara kubwa au ndogo ukicheza kidogo tu unahesabu maumivu .kidogo ajira huwa zinatulinda wavivu na wazembe ukikosea unaonywa.

4: Biashara ni upepo. Nikitumia neno "upepo " wafanya biashara wananielewa, yani unaweza kimbiza leo kesho ukabuma, unaweza ukapata losi mwaka huu ila mwakan ukatoboa. Wakati waajiliwa ni mkataba tu ndo unaamua hatima yako.

5.: Biashara inakulazimisha kufikilia baada yakufikilia, kufanya baada ya kufanya. Kila siku uwe na wazo jipya uwe na mtandao mpya na uwe na bidhaa mpya. Hivyo kila ukimaliza kuwaza hili linakuja lingine. Wasomi wengi makazini mkisha saini daftar la mahudhurio tayari umemaliza siku, kuwaza atawaza bossi .

Hii ndo sababu kubwa ya wafanyakazi kuogopa biashara au kufanya bila mafanikio. Ndugu zangu tusijazane ujinga biashara sio kama mnavyozijadili mitandaoni , biashara sio kama mnavyosoma kwenye vitabu , biashara sio kama mnavyoandika kwenye makaratasi laa hasha biashara ni uthubutu , kujiamini na kujitoa . Nisitofasirike vibaya simaanishi waajiliwa hatuwezi biashara ila namaana mitazamo ya wasomi /waajiliwa kuhusu biashara ni ya nadharia ambayo haiyendani na uhalisia.

Tofauti hizi ni kwa uchache tu mwenye zingine aongezee.
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa UHURU ukiwa mfanya biashara/ umejiajiri unakuwa na uhuru wa kusimamia mawazo yako na kile unachokiamini

Pia hata faida yote utakayoipata ni yako ila kazini mnaweza ingiza faida ya bili 1 mfano wewe ukaambulia laki 7.......

Nimeacha kazi toka jana hahahaha nimejiajiri tayari
 
mkuu kuna kitu kinaitwa UHURU ukiwa mfanya biashara/ umejiajiri unakuwa na uhuru wa kusimamia mawazo yako na kile unachokiamini

Pia hata faida yote utakayoipata ni yako ila kazini mnaweza ingiza faida ya bili 1 mfano wewe ukaambulia laki 7.......

Nimeacha kazi toka jana hahahaha nimejiajiri tayari
We unaweza nisaidia kuwaelezea watu ulivyokuwa ukiichukulia biashara kipindi umeajiriwa na baada yakuingia rasmi, Mana ndio mzizi wa mada yangu apo mkuu
 
Usitukane mamba kabla hujavuka mto.

Kuwa na akiba ya maneno.
Mkuu kwanza sijacheka ajira ila nimwjicheka kuwa nimeacha kazi toka jana....pia nimeweka msingi mkubwa wala siwezi kufeli maana kuna biashara nilianza kipindi cha corona imenipa ujasiri zaidi na kuna ufugaji japo siuchukulii serious sana but pia ninataka nianze biashara mpya soon so napambana na sioni aibu kukaa barabarani kutembeza machungwa.....
 
We unaweza nisaidia kuwaelezea watu ulivyokuwa ukiichukulia biashara kipindi umeajiriwa na baada yakuingia rasmi, Mana ndio mzizi wa mada yangu apo mkuu
Mkuu binafsi nilikuwa naona biashara inalipa ila sasa inahitaji kujilipua maana kwenye kuajiriwa hata iwaje mshahara unapata bila shida yoyote....

Pia binafsi nimeamua kujiajiri baada ya kuona mshahara wangu ni mdogo yani take home laki 5 baada ya makato kadhaa na hapo kuvunja mkataba inaweza kunicost hadi 12mil.....ila mtu kama anapata mshahara mzuri kama mil 1 take home or laki 8 au mil 2 huko sioni shida kuajiriwa mkuu....

Biashara nayo inaogopesha na inahitaji sana kuondoa aibu maana ukiwa kazini unaile status yako umejiwekea hata mtaani visuti vizuri ghetto lako huna habari.....
 
Mkuu binafsi nilikuwa naona biashara inalipa ila sasa inahitaji kujilipua maana kwenye kuajiriwa hata iwaje mshahara unapata bila shida yoyote....

pia binafsi nimeamua kujiajiri baada ya kuona mshahara wangu ni mdogo yani take home laki 5 baada ya makato kadhaa na hapo kuvunja mkataba inaweza kunicost hadi 12mil.....ila mtu kama anapata mshahara mzuri kama mil 1 take home or laki 8 au mil 2 huko sioni shida kuajiriwa mkuu....

biashara nayo inaogopesha na inahitaji sana kuondoa aibu maana ukiwa kazini unaile status yako umejiwekea hata mtaani visuti vizuri ghetto lako huna habari.....
Ujue sometime biashara znakuchapa mpaka unatamani ajira hata ya laki 4. wengi wana passion ya kufanya biashara lakn changamoto n nyng mno ndo mana wanaamua kubakia ajiran.

Sometime mtu anafanya biashara inamchapa hadi mtaji unakata ....kwa nn asitaman ajira
 
ujue sometime biashara znakuchapa mpaka unatamani ajira hata ya laki 4. wengi wana passion ya kufanya biashara lakn changamoto n nyng mno ndo mana wanaamua kubakia ajiran. sometime mtu anafanya biashara inamchapa hadi mtaji unakata ....kwa nn asitaman ajira
Ni kweli mkuu kuna pesa ukiipata kwenye mshahara basi sio lazima uache ufanye biashara...sasa just inagine mtu ana laki 2 why asiache apigane na biashara ....
 
Kuwa na mahela ya masharti masharti na kujibana bana bora nibaki na hela zangu za ngama tu,ni-enjoy coz we only live once na ukifa hela zako watazitumbua like nobody business
Ni kweli mkuu na ndio maana yeye akifikisha miaka 47 ata retire na kurudi zake kijijini wkt wewe/sisi wasomi tunasubiri tufike miaka 60 tuanze kupambana na NSSF kuhusu mafao yetu huku tukiambiwa kuna michango yako haikuwasilishwa na mwajiri wako,hebu kaifuatilie kwanza.
 
Katika maisha yangu nilishajiapiza pesa za masharti Big NO nahitaji uhuru WA akili na mwili ni heri nishiriki ujambazi nipate pesa zisizo na masharti ya matumizi kuliko ndagu
 
Sasa nenda kamtembelee mwenye PhD,bachelor au master's. Kwanza utamkuta ana bonge la diary limejaa mipango tu, akianza kuongea kila aina ya biashara yeye anaijua wakati hajauza hata maji.
Hahah naona umeamua kutuchana 'wasomi' na mipango yetu mzee baba.
 
Back
Top Bottom